Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, November 9, 2014

Korea Kaskazini yawaachia huru Wamarekani

Matthew Miller(kushoto)Jeffrey Fowle (Katikati) Kenneth Bae (Kulia) Wamarekani walioachiwa huru na Korea Kaskazini
Matthew Miller(kushoto)Jeffrey Fowle (Katikati) Kenneth Bae (Kulia) Wamarekani walioachiwa huru na Korea Kaskazini
Maafisa wa Marekani wanasema Korea Kaskazini imewaachia huru Wamarekani Kenneth Bae na Matthew Todd Miller na kwamba wawili hao wako njiani kurudi nyumbani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki  alitoa taarifa  hiyo Jumamosi akikaribisha kuachiwa kwao.
Alisema mkurugenzi wa idara ya kitaifa ya ujasusi James Clapper alijadilia swala la kuachiwa kwa Wamarekani hao wawili na maafisa wa Korea Kaskazini. Marekani kwa muda mrefu imetoa mwito kwa Korea Kaskazini kuwaachia huru  Wamarekani hao kwa misingi ya kibinadamu.
Tangazo la kuwaachia huru Bw. Bae na Bw. Miller limetolewa wiki chache baada ya hatua isiyotegemewa ya kumwachia huru M’marekani mwingine Jeffrey Fowle aliyekuwa kizuizini huko Korea Kaskazini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment