Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Saturday, November 8, 2014

Jaji Warioba ni shujaa atakayeheshimika vizazi vijavyo


Jaji Warioba akifafanua jambo 
Mwananchi
Mhariri,

Jaji Warioba ni shujaa hana sababu yoyote ya kuona aibu. Asikate tamaa bali tukio kama hili ndio liwe kichocheo kwake, kuweka juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi waielewe vizuri katiba inayopendekezwa, ili iwarahisishie kufanya uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura.

Viongozi wa vyama vya upinzani, fursa hizo mnaongezewa kuwafikishia ujumbe wananchi. Mshindwe tu wenyewe kuufikisha ujumbe huo kwa wenye nchi, halafu msiwageuke wananchi na kuanza kuwalaumu kama ujumbe wenu hauwafikii ipasavyo.

Watanzania sio wapumbavu wala sio wajinga. Mwalimu Nyerere alipozunguka nchi nzima kutafuta uhuru walimuelewa vizuri sana na matokeo yake yalionekana.

Nyinyi pia nendeni kwa wananchi hao hao, waelezeni yote upungufu uliopo waelewe. Wao pekee ndiyo wenye uamuzi wa mwisho. Tumieni fursa hizi vizuri kuwaelimisha wananchi.

Edmund Charles,

Dar es Salaam.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment