Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, November 4, 2014

Al-Shabab watishia kushambulia Burundi

Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
Mji mkuu wa Burundi, BujumburaMarekani imewaonya raia wake wasiende Burundi na kuwashauri wafanyakazi wa serikali ya Marekani walioko nchini humo kuchukua tahadhari haswa nyakati za usiku.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imewaonya raia wote wa Marekani wasiende Burundi, ila kwa shughuli muhimu sana, ikisema kuwa kuna vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Somalia-al Shabab, pamoja na uhalifu wa hali ya juu ndani ya taifa hilo maskini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kundi la al-Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya Burundi na huenda likalenga maslahi ya Marekani.
Onyo hilo linaonya Wamarekani walioko Burundi wasitumie barabara kuu kuanzia jioni hadi alfajiri. Inasema magenge yenye silaha huvizia magari kwenye barabara kuu zinazoingia mji mkuu Bujumbura
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment