Writen by
sadataley
1:33 PM
-
0
Comments
PROFESA Karim Hirji, katika kitabu kinachoeleza maisha yake kiitwacho, Growing Up with Tanzania, ametoa dhana nzuri kuhusu mapito ambayo maisha ya mtu yanakutana na ya mtu mwingine au taasisi kuliko kawaida.
Naazima dhana hiyo hiyo leo katika kueleza namna maisha yangu na Profesa Ali Mazrui aliyefariki dunia Oktoba 12 mwaka huu katika eneo la Binghamton, New York, Marekani yalivyokutana na kukua pamoja. Alifariki akiwa na umri wa miaka 81 na miezi nane.
Namkumbuka Mazrui, niliyekuwa nikimwita Mjomba Ali, katika muktadha wa midahalo mbalimbali iliyokuwa ikifanyika katika Vyuo Vikuu vya nchi za Kenya, Uganda na Tanzania katika miaka ya 1960 na 1970 ambayo ilikuwa mikali kiitikadi na kisiasa.
Kulikuwa na Wahadhiri waliokuwa wakipendelea sera za kimagharibi, wengine kimashariki na walikuwapo waliokuwa na msimamo wa kati. Ikumbukwe kwamba huu ulikuwa ni wakati wa Vita Baridi na hali hiyo iliakisiwa katika midahalo hiyo kisomi, kiitikadi na kisiasa.
Midahalo hii ilikuwa ikifanywa na wasomi magwiji wa Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla. Hapa nazungumzia watu wa kariba ya Walter Rodney, Giovanni Arrighi, A J Temu, Justinian Rweyemamu, John Saul, Tamas Sczentes, Yash Tandon, Abdalla Bujra na Mahmood Mamdani.
Wengine ni Hirji, Issa Shivji, Dani Nabudere, Omwony Ojok, Henry Mapolu, Aki Sawyerr, Kwesi Botchwey, Marjorie Mbilinyi, Yash Pal Ghai, Dharam Ghai, John Samuel Mbiti, Okot p’Bitek, Ngugi wa Thiong’o, Micere Mugo, Sol Piciotto na wengine wengi.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiligeuka kuwa eneo Takatifu kwa wapigania Uhuru kutoka karibu nchi zote za Afrika na wanaharakati wa Dunia. Ilikuwa jambo la kawaida kupishana na kujadiliana na wawakilishi kutoka vyama vya ANC, Frelimo, Swapo, Polisario, PLO, Black Power na Black Panthers, nikitaja vichache tu miongoni mwa vingi katika eneo la chuo.
Aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere, ndiye aliyengeneza mazingira hayo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yeye mwenyewe akiwa chachu ya midahalo hiyo kwa kutoa miongozo mbalimbali iliyohitaji uchambuzi wa kina kisomi, kisiasa na kiitikadi.
Kimsingi, hakukuwa na chuo kingine kikuu ambacho mtu angetamani kusoma kuliko cha Dar es Salaam katika miaka ya 1960 na 1970. Binafsi, najiona mwenye bahati sana kuwa mwanafunzi wa chuo hicho katika wakati huo.
Kukutana mara ya kwanza na Mazrui
Mara ya kwanza nilikutana na Mjomba Ali mwaka 1969 wakati mimi nikiwa mwanafunzi Dar es Salaam naye akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na alikuwa amekuja kuhudhuria mkutano.
Wakati huo, mikutano ya kitaaluma ilikuwa jambo la kawaida chini ya mfumo uliokuwepo ambao vyuo vyote vilikuwa chini ya kilichoitwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki. Nilikuwa nikihudhuria mikutano hiyo na kumshuhudia Mazrui akiwasilisha mada zake.
Kwa ufupi tu niseme kwamba wakati huo nilikuwa nikimshuhudia na kumuona msomi wa kiwango cha juu, mtunga maneno, mzalendo na mwana majumui wa Afrika katika ubora wake wa kiwango cha juu.
Katika uungwana wake na kujishusha, miaka mingi baadaye, siku moja mjomba wangu huyu wa hiari alipata kuniambia kwamba anakumbuka kuwahi kushindwa katika mojawapo ya midahalo yake na Walter Rodney mnamo mwaka 1970 chuoni Makerere.
Wakati nikitafakari kuhusu midahalo iliyokuwa ikifanyika wakati huo, ni rahisi kwangu kubaini kwanini Mazrui aliyekuwa na mrengo wa kati alikuwa na wafuasi wengi miongoni mwa wanafunzi.
Wakati huo, mijadala ya kiitikadi mingi ilikuwa kati ya mrengo wa kulia na kushoto na ilikuwa mikali sana; wakati mwingine ikitumia lugha kali, katili na ikifuatwa kama dini.
Wanafunzi waliotaka kusikia na kutafakari kuhusu pande zote kinzani walikuwa wanampenda Mazrui kwa vile aliwapa msimamo ulio wa kati. Jambo la kuvutia kwa mjomba wangu lilikuwa kwamba alibaki katika msimamo huo kwa muda mrefu, akiwaacha wahadhiri wenzake wakihama kutoka kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto mara kwa mara.
Hadi sasa, bado dunia inatafuta mfumo ambao utafaa kwa wote. Ule msemo maarufu ambao tulikuwa tukiutumia wakati ule; Aluta Continua, bado una maana hadi leo.
Hakutaka kuandika kitabu cha maisha yake
Mimi na mtoto wa Mazrui, Alamin Mazrui, tulijaribu sana kumshawishi Profesa akubali ama kuandika mwenyewe au kuandikiwa kitabu cha historia ya maisha yake. Haikuwa siri kwenye hili kwani tuliwahi hata kumwambia.
Hakutaka kutukatalia waziwazi, lakini ninapotafakari sasa naona kama hakutaka kuandikiwa kitabu. Hata hivyo, hakutukatalia kabisa kwani alikubali tuchapishe baadhi ya mijadala yake aliyowahi kuifanya na wasomi mbalimbali na tulifanikiwa kutengeneza kwa kuchapa kitabu chenye sehemu tatu.
Sasa nafahamu kwamba Mjomba hakuwa na nia yoyote ya kuandika au kuandikiwa kitabu. Mimi na Alamin tulipaswa kulifahamu hili wakati tukihariri midahalo yake mbalimbali kwenye kitabu tulichochapa.
Kama wewe ni msomi wa kiwango cha juu, ina maana maandishi yako yatakuwa yanajadiliwa mara kwa mara na nyakati zote. Maneno yako yatakuwa yanazungumzwa na kuelezwa miaka mingi baada ya wewe kuwa umeondoka duniani.
Sasa kama hali yenyewe ndiyo hiyo, una haja gani ya kutengeneza kijitabu ambacho kitakuwa kinarudia au kinaeleza kwa uchache tu yale ambayo yanajadiliwa, kukosolewa na kuongezwa nyama kila wakati? Hata kama ni picha, kitabu hicho kitatumia picha zile tayari zimetumika kwingineko.
Kama Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama ya Juu ya Kenya, nilipata bahati ya kutembelewa na Mazrui na Profesa Robert Martin ofisini kwangu mwaka jana. Mjomba Ali alipata fursa ya kuzungumza na majaji kuhusu sheria na siasa chini ya Katiba Mpya ya Kenya ya mwaka 2010.
Huu ulikuwa ni wakati mwafaka, hususani kwa majaji ambao kwao “Sheria ni sheria, ni sheria na sheria”. Kwamba Katiba Mpya ya Kenya si kitu ambacho ni sheria pekee bali inahitaji weledi mtambuka wa masuala mbalimbali katika kuitafsiri na kuitekeleza.
Kama Mwafrika ninayeamini katika mizimu ya mababu zetu, ninaamini kwamba roho ya Mjomba Ali itaendelea kutulinda na kukua pamoja nasi katika maisha yetu. Nina uhakika mijadala kuhusu kazi zake alizofanya hapa duniani itaendelea kuwepo karne nyingi kutoka sasa.
Ninamuombea kwa Mungu kwamba akutane tena na Walter Rodney ili waendeshe mdahalo mwingine hadi mshindi halali apatikane.
Allah na ailaze roho yake mahala pema peponi. Amen

No comments
Post a Comment