Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, September 20, 2014

Polisi Dar wapingwa kila kona



Waandishi wa  habari, wakiwa wameanguka chini, katika makao Wizara ya Mambo ya Ndani, Dar es Salaam juzi, wakati Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakupotumia nguvu dhidi ya wanahabari waliokwenda kufuatilia yaliyojiri baada ya mahojiano ya mwenyekiti wa  Chadema Freeman Mbowe,  na Jeshi hilo kwenye Polisi. Picha na Said Khamis  
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar\Mikoani. Kitendo cha Jeshi la Polisi kuzidi kuwapiga waandishi wa habari wakiwa kazini kimelaaniwa vikali na taasisi mbalimbali, huku Chadema kikisisitiza kutositisha mpango wao wa kuandamana nchi nzima kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.


Tukio la kushambuliwa kwa waandishi watatu lilitokea juzi mbele ya ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, kutaka kufahamu hatima ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa anahojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kutokana na kauli aliyoitoa ya kuitisha maandamano nchi nzima yasiyo na kikomo kupinga kile kinachoendelea bungeni Dodoma.

Waandishi waliokutana na kadhia hiyo ni wa gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango, gazeti la Hoja, Shamimu Ausi na mpiga pichawa magazeti ya Serikali (TSN), Yusuf Badi ambao walijeruhiwa. Isango alijeruhiwa mguuni na Ausi usoni karibu na jicho.
Kitendo hicho kimetokea zikiwa zimepita siku mbili tangu kufanyika mkutano wa mashauriano kati ya vyombo vya dola na waandishi wa habari ambapo Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal alikuwa mgeni rasmi. Katika mkutano huo, si viongozi wa polisi au wawakilishi wake waliohudhuria huku Dk Bilal akitoa wito kwa vyombo hivyo kufanya kazi kwa kushirikiana bila kukwaruzana kwa lengo la kudumisha amani.
Tamko la TEF

Jana Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lilitoa kauli ya kulaani shambulio hilo kwa wanahabari na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu kulifumua jeshi hilo na kuliunda upya.

Aidha, TEF wamesema watamwandikia barua IGP juu ya kulaani tukio hilo na kumtaka kuchukua hatua dhidi ya polisi wake waliotekeleza vitendo hivyo kutokana na kujulikana kupitia picha za video na mnato zilizopigwa.

Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda alisema Jukwaa linalaani juu ya kitendo hicho na kwamba polisi yeyote mwenye silika za ukiukwaji wa haki za binadamu zikiwamo za namna hiyo ya kuwashambulia wanahabari si tu anakwenda kinyume na wajibu wake wa kikazi wa kukabiliana na uhalifu, bali yeye mwenyewe ana vimelea vya uhalifu.
“Jeshi la Polisi linapaswa kufanya kama kile kilichofanywa na polisi wenzao wa Brazil, Julai mwaka huu ambako askari polisi wanne walionaswa katika mikanda ya video wakiwashambulia waandishi wa habari walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kufanyika,” alisema Kibanda.

Baraza la Habari

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga alisema hatua hiyo ya polisi kuwashambulia waandishi wa habari kwa virungu, mateke na kutishiwa au kusakiziwa mbwa na kukimbizwa imekuja siku moja baada ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal kuvitaka vyombo vya ulinzi na sheria kushirikiana na vyombo vya habari katika kufanya kazi kwa ajili ya kuendeleza na kulinda amani ya nchi.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment