Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, September 20, 2014

Askofu Bagonza: Mipaka ya nchi siyo salama


Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheran Tanzania (KKKT) Dk. Alex Malasusa, ambaye yupo Sumbawanga kwa ajili ya kikao cha Halmashauri kuu ya Kanisa hili. Picha na Maktaba 
Na Mussa Mwangoka, Mwananchi.
Sumbawanga. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe Dk.Benson Bagonza ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ambazo Serikali inachukua katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa Ebola kwenye mipaka ya Taifa.

Askofu huyo alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viunga vya Kanisa la KKKT Usharika wa Sumbawanga ambapo kikao cha halmashauri kuu ya kanisa hilo kinafanyika na kuwajumuisha maaskofu 23 kutoka dayosisi zote nchini wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk. Alex Malasusa.

Alisema mipaka ya nchi si salama katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa huo, kwani kama vitu visivyotakiwa vinaweza kupita mipakani ni rahisi kwa vidudu vilivyo mwilini kwa mtu kuweza kuingia na kusababisha kuenea kwa ugonjwa huo ambao ni tishio na umeua watu wengi katika Nchi za Afrika Magharibi.
Aliitaka Serikali kuchukua tahadhari ya kutosha ili kudhibiti ugonjwa huo usipenye na kuingia nchini, kwani mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani hususani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Tanzania ni mkubwa na katika nchi hiyo tayari watu kadhaa wamefariki dunia kutokana na maradhi hayo.
Pia, alisema fungamano la makanisa ya Afrika wamepanga kuweka sadaka maalumu Septemba 28 ili kuchangia wale walioathirika na ugonjwa huo hususani katika nchi za Afrika Magharibi ikiwamo DRC.

Wakati askofu huyo, akieleza hayo tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tayari imesambaza na kufunga vifaa vya kupimia joto (Thermal Scanner) katika mipaka ya nchi ili kudhibiti kuenea ugonjwa huo.

DRC inakuwa nchi ya tano Afrika kukumbwa na mlipuko huo ambao hadi sasa umeua zaidi ya watu 2000 Magharibi mwa Afrika.
Nchi nyingine Afrika zilizokumbwa na Ebola ni Liberia, Nigeria, Sierra Leone, Guinea na DRC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment