Writen by
sadataley
2:55 PM
-
0
Comments
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha
alisema jana katika ibara ya 19 hawakupata theluthi mbili ya kura
zilizopigwa kutoka Zanzibar.
Pia Nahodha alisema kamati yake ilikosa theluthi mbili ya kura zilizopigwa kwa upande wa Tanzania Bara katika ibara ya 22.
Alisema katika ibara ya 19 ambayo alikosekana mtu mmoja kutimiza theluthi mbili ya kura kwa upande wa Zanzibar.
Ibara hiyo inatamka kuwa kiongozi wa umma
hatatumia ama kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali za umma zikiwamo
zilizokodishwa kwa Serikali kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi ama
kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.
“Kilichofanyika katika rasimu hii kulikuwa na neno
kiongozi wa umma sasa wajumbe walio wengi wakafanya marekebisho kuwa si
suala la kiongozi tu wa umma anayepaswa kuzingatia hili hata watumishi
wa umma,” alisema.
Alisema kutokana na hoja hiyo wajumbe walio wengi
wakaongeza neno mtumishi wa umma, jambo ambalo lilikataliwa na mjumbe
mmoja kutoka Zanzibar ambaye alitaka ibara hiyo kusomeka kama ilivyo
katika Rasimu ya Katiba.
Nahodha alisema kwa upande wa ibara ya 22, wajumbe walio wengi walitaka ibara hiyo ihamishiwe katika sura ya 11.
Ibara hiyo inahusiana na watumishi wa umma aliye
katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine ya
kudumu yenye malipo ya mshahara.
Pia ibara hiyo inasema mtumishi wa umma
atakayeamua kugombea, kuchaguliwa na kuteuliwa kushika nafasi ya
madaraka ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hiyo au uongozi wa
ngazi yoyote katika chama cha siasa mtumishi huyo atachukuliwa kuwa
utumishi wake umekoma tangu siku ya kuteuliwa kugombea, kuchaguliwa au
kuteuliwa kushika nafasi ya madaraka ya kisiasa au uongozi katika chama
cha siasa.
Nahodha , alisema mjumbe mmoja alipinga kuhamishwa kwa ibara hiyo katika sura ya 11 na kutaka ibakie katika sura hiyo.
Aidha, Nahodha alisema kulikuwa na mjadala wa kina kuhusiana na ibara zinazohusiana na rushwa.
No comments
Post a Comment