Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 14, 2014

Ujerumani yaweka historia Kombe la Dunia, Goetze aizamisha Argentina


Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia na Kombe la Dunia mara baada ya ushindi wao katika mechi ngumu dhidi ya Argentina kule Maracana, Rio de Janeiro jana. PICHA | AFP 
Na Mwandishi Wetu/AFPRio de Janeiro, Brazil. Goli la Mario Goetze katika dakika ya 113 jana limeiwezesha Ujerumani kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia kwa mara ya nne katika uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro.
Goli hilo pekee la mechi pia limeiwezesha Ujerumani kuandika historia kwa kuwa timu pekee toka Ulaya iliyoweza kutwaa Kombe la Dunia katika kipute kilichopigwa Amerika Kusini.
Goetze, ambaye ni straika wa Bayern Munich, alizamisha ndoto za Muargentina Lionel Messi za kuakisi mafanikio ya mkongwe mwingine wa Argentina, Diego Maradona, aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1986.
Dakika muhimu ya mchuano huo Jumapili ilidhihirika mbele ya mashabiki karibu 75,000 katika uwanja maarufu wa Maracana, pale Andre Schuerrle alipochomoka toka kushoto, akimpigia pande Goetze.
Mwana-Bayern huyo mwenye umri wa miaka 22  alituliza mpira kifuani kwa kujiamini, huku akijipinda na kufyatua kigongo kikali kilichomwacha kipa wa Argentina, Sergio Romero, akitoa macho.
Uwanja mzima uliokuwa umejaa mashabiki wa Ujerumani ulilipuka kwa shangwe wakati nyavu za Argentina zikitikisika.
Messi na vijana wake walibanwa mbavu, wakipoteza nafasi chache za kufunga walizoambulia katika mchuano huo wa miamba waloonekana kuwa nguvu sawa.
Fowadi huyo anayeichezea Barcelona atakumbukwa kwa kushidwa kutumia ‘mchongo’ alotengenezewa katika kipindi cha pili, huku akipiga nje ‘free kick’ walopata Argentina dakika za mwisho mwisho.
Ushindi wa Ujerumani jana ulishangiliwa vilivyo na mashabiki wa Brazili, ambao hawakufurahishwa na uwezekano wa mahasimu wao, Argentina, kuchukua Kombe hilo la Dunia huku Selecao wakiwa wameshindwa hata kuambulia nafasi ya tatu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment