Writen by
sadataley
5:21 PM
-
0
Comments
Na Ibrahim Yamola na Exuper Kachenje, MwananchiDar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete kujitokeza hadharani kutafuta suluhu ya kupata mwafaka wa mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa hakuna mamlaka nyingine zaidi inayoweza kuunusuru.
Pia, amewatahadharisha viongozi wa dini kuwa
makini na kauli zao wanazozitoa za kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni Agosti 5.
Dk Slaa aliyasema hayo juzi katika mahojiano
maalumu na gazeti hili, makao makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa, Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
“Mwenye rungu la kuweza kutengua kitendawili hiki
ili turudi bungeni ni Rais (Kikwete) mwenyewe, hakuna mwingine,”alisema
Dk Slaa.
“Tatizo aliyesaini waraka uliowasilishwa na
Warioba ni Rais mwenyewe, alisaini ukurasa wa kwanza na wa mwisho, kwa
taarifa rasmi za kina Warioba, Rais alishirikishwa na Tume ya Mabadiliko
ya Katiba hatua kwa hatua na kwa kila hatua alisema sawa mchakato
uendelee,”alisema Dk Slaa.
Alikumbusha kuwa wakati akipokea Rasimu ya Pili ya
Katiba, Rais Kikwete alisema: “Mtapata rasimu, ijadilini na itapitishwa
na Bunge. Kwa mwanasheria yeyote, lugha kujadiliwa na kupitishwa haitoi
ruhusa ya kubadilishwa, inatoa ruhusa kuboreshwa. Ndiyo utaratibu wa
sheria zote duniani.”
“Sasa anapofika mahali anayeleta wazo ni Rais,
lakini kwa bahati mbaya anayekwenda kupindua pia ni Rais na amekwenda
mbali zaidi kiasi cha kusema kwamba kama Serikali tatu ile ile ambayo
yeye ameisaini itapatikana, jeshi litapindua nchi.
“Anayezungumza ni Rais, hakuna mamlaka nyingine
inayoweza kutengua kitendawili hiki. Wanaweza kuja maaskofu,
...masheikh, asasi mbalimbali... hatimaye hakuna anayeweza kutengua kwa
sababu aliyeufanya ni mwenye mamlaka ya juu,”alisema.
Dk Slaa aliyewahi kuwa Mbunge wa Karatu kwa
vipindi tofauti alitaja mambo matano anayopaswa kuyafanya Rais Kikwete
ili wajunge wa Bunge Maalumu la Katiba wanaounda Ukawa waweze kurejea
bungeni.Aliainisha la kwanza ni majadiliano kuwa na misingi iliyo wazi
akisema Ukawa haipo tayari kufanya mambo na kuishia kupewa pipi na
kwamba Katiba Mpya lazima ipatikane kwa maridhiano.
Alitaja jambo la pili kuwa ni lazima wao , Ukawa
wahakikishiwe kuwa kanuni hazichezewi baada ya kupitishwa na siyo kama
ilivyofanya CCM, baada ya Ukawa kutoka bungeni akisema hatua hiyo ni
sawa na uhuni. Lingine ni kuhakikishiwa kitakachojadiliwa ni rasimu
iliyowasilishwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba si kingine.
Huku akitoa mfano wa hotuba ya Mwalimu Julius
Nyerere ya Juni, 1965 akisema ndiyo iliyowajibu CCM kuhusu msimamo wa
Serikali mbili waliodai ni kuenzi aliyoanzisha Nyerere, Dk Slaa alisema;
“Itakuwa upumbavu kama watu wataamini kwamba
katiba haibadiliki, hata kama imedhihirika kuwa haitoshelezi tena haja
ya wananchi kwa wakati ule.”
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Slaa--Rais-Kikwete-ana-rungu-la-Katiba-Mpya/-/1597296/2373664/-/3ethpz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Slaa--Rais-Kikwete-ana-rungu-la-Katiba-Mpya/-/1597296/2373664/-/3ethpz/-/index.html
No comments
Post a Comment