Writen by
sadataley
6:20 PM
-
0
Comments
Mchezaji wa zamani wa timu ya
taifa ya Kenya, Harambee Stars, Mike Okoth amesema hatamzuia mwanawe
Divorc Origi kujiunga na Liverpool kwa kitita cha pauni milioni kumi.
Lakini Okoth amesema watajadialiana mambo kadhaa
pamoja na timu zingine ambazo zinataka kumsajili Origi ambaye
aliiwakilisha Ubelgiji kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini
Brazil.Mbali na Liverpool timu zingine za ligi kuu ya England ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili Origi ni Tottenham Hotspur na Arsenal lakini hawajataja kiasi cha fedha mbazo wako tayari kutoa.
Akizungumza na BBC Jumatatu wiki hii kwa njia ya simu akiwa Ubelgiji, Okoth, ambaye alihudhuria mashindano ya kombe la dunia anasema:”
Okoth amesema kuwa bado anamsubiri kijana arudi kutoka Ubelgiji kisha azungumze naye.
''Yeye ni mtu mzima mwenye uwezo wa kujiamulia mengine. Kuna timu kutoka Ujerumani, Italia na Hispania ambazo zimewasiliana nasi kupitia wakala wao.Itabidi tuchunguze uzito wa timu hizo na makocha wanaozifunza,’’ alisema babake Origi.
'Klabu ya kumkuza Origi'
''La mhimu ninalotaka ni ajiunge na klabu itakayomkuza na apate fursa nzuri ya kujiendeleza. Sitafurahia ajiunge na klabu ambayo hatapata muda wa kutosha wa kucheza hata kama pesa ni nyingi. Siangalii tu pesa lakini nalenga mbele kimchezo.Anaweza kujiunga na klabu inayotoa pesa nzuri za kuhama lakini singetaka mara tu akivuka aanze kujuta kama hachezi mara kwa mara.’’
Kwa sasa Origi anaichezea Lille ya Ufaransa lakini anasema lengo lake kubwa ni kushiriki ligi kuu ya England.
Okoth anasema licha ya kwamba yeye ni shabiki wa Liverpool watazungumzia zaidi mambo mengine na Origi akirudi Ubelgiji kutoka Brazil ambako aliiwakilisha taifa lake alikozaliwa na kufurahisha wengi wakiwemo mashabiki wa Kenya ambao baadhi yao walibubujikwa na machozi Ubelgiji ilipong’olewa na Argentina kwenye mechi ya robo-fainali ambayo walipoteza kwa bao 1-0.
No comments
Post a Comment