Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 11, 2014

Riek Machar asema hana uchu wa madaraka


Riek Machar anasema kuwa wananchi wanapigania uhuru wao
Aliyekuwa makamu wa Rais Nchini Sudan Kusini,Daktari Riek Machar, anasema kuwa anachozungumzia kwa sasa ni kukubaliana na sera ya mfumo mpya wa uongozi wa taifa hilo inayokubaliana na mgogoro wa kisiasa.
Machar sasa anaongoza vita vya upinzani dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Anasema kuwa anapigania mageuzi wala sio kutaka wadhifa katika utawala wa sasa.
Riek Machar ameiambia BBC kuwa mfumo huo unastahili kufaidi kila mtu Nchini humo na kuonyesha kuwa nchi hiyo ina demokrasia
Mwezi uliopita serikia na waasi walikubalina kuunda seriali ya umoja wa kitafa katika kipindi cha siku sitini.
Lakini baada ya kuulizwa ikiwa hilo litafanyika bwana Machar alikataa kujibu.
Sudan Kusini ilipata uhuru miaka mitatu iliyipita lakini mwaka uliopita ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment