Writen by
sadataley
4:07 PM
-
0
Comments
Na Nuzulack Dausen, MwananchiDar es Salaam. Mchakato wa kutafuta kampuni 100 bora za kiwango cha kati nchini kwa mwaka huu, umeanza na kampuni mbalimbali zitafanyiwa utafiti kubaini viwango vyao vya ukuaji kibiashara.
Utafiti huo ambao hufanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kupitia gazeti la The Citizen
pamoja na Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu ya KPMG, unalenga kubaini
kampuni zinazokua haraka kwa kuonyesha ubora wa biashara na kuweka
bayana baadhi ya taarifa za mafanikio yao.
MCL inachapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen.
Utafiti huo wa nne tangu kuanza kwake mwaka 2011
unazipanga kampuni kulingana na ubora katika nyanja za ukuaji wa mapato,
faida, marejesho kwa wabia na uzalishaji wa fedha taslimu.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana, mkurugenzi
mtendaji wa KPMG, David Gachewa alisema kampuni bora katika utafiti huo
ni zile zilizofanikiwa kukuza nafasi yake katika masoko na baada ya
muda maendeleo yanayosu marejesho kwa wabia na kuwa na hali nzuri
kifedha.
Alisema utafiti wa mwaka huu utafanywa na taasisi
ya Research Solutions Africa ambayo itahusika kupokea fomu za maswali
wakati KPMG itapokea na kuzichambua taarifa za kifedha.
Pia, utafiti huo umepata mdhamini mpya ambaye ni
Bank M ambayo itadhamini kwa miaka mitatu mfululizo hadi 2016 kwa Dola
100, 000 za Kimarekani (Sh165 milioni) kila mwaka.
“Kwa wanaoshiriki, utafiti huu unatoa fursa ya
kushiriki kwenye maendeleo ya hifadhi ya taarifa za sekta na zaidi
kujipima na wengine,” alisema.
“Wale watakaoingia kwenye orodha ya kampuni 100
bora watanufaika kwa kujulikana kuwa kampuni zilizofanya vizuri nchini
na kisekta na kuingizwa katika klabu yenye hadhi ya waanzilishi wenye
ustawi,” alisema Gachewa.
Aliongeza kuwa kampuni yoyote inaweza kushiriki
kwa hiari isipokuwa benki, kampuni za bima, uhasibu, taasisi za ushauri
wa kifedha na kampuni za sheria.
Mwenyekiti wa Bank M, Nimrod Mkono alisema benki
yake itaendelea kusaidia jamii ili kuleta maendeleo nchini na kuongeza
kuwa tayari benki hiyo ina miradi mbalimbali ya kijamii ambayo wao
wanaiona ni sehemu ya utekelezaji wa nia njema.
Kwa upande wake, ofisa mwendeshaji wa MCL, Francis
Nanai aliishukuru Bank M kwa udhaamini wake wa kuinua kampuni za kati
na ndogo katika jitihada za kuleta maendeleo .nchini.
No comments
Post a Comment