Writen by
sadataley
1:23 PM
-
0
Comments
Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya
muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia
kwa mikwaju ya penalti.Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.
Wafungaji wa Argentina walikuwa ni Lionel Messi,Ezequiel Garay Sergio Aguero na kisha Maxi Rodriguez.
Argentina sasa Itachuana na Ujerumani ambayo iliweka historia kwa kuinyuka Brazil mabao 7-1katika nusu fanali.
Brazil ilipata kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne.
Penalti ndizo zitakazoamua nani kati ya Uholanzi na Argentina atakutana na Ujerumani katika fainali.
00:45 Mpira umekwisha .Sasa ni dakika 30 za muda wa ziada.
00:42 Argentina 0-0 Uholanzi 82''
00:40 Argentina wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa mpigo.
00:06 Demichelis anaoneshwa kadi ya Njano baada ya kumwangusha Arjen Robben
00:05Uholanzi 0-0 Argentina 45'' Kipindi cha pili kimeanza .
23:45 +1 Kufikia wakati kama huu hapo jana Ujerumani ilikuwa imemfunga Brazil mabao 5-0
23:44 Martins Ndi (uholanzi) aoneshwa kadi ya kwanza ya manjano
23:23 Kona nyengine kuelkea upande wa Uholanzi ,duh unatoka nje na inakuwa ni Goalkick
23:20 Kona ya kwanza kuelekea upande wa Uholanzi,,,lakini Wapi inazimwa
23:20 Argentina 0 -0 Uholanzi
23:14 Messi ndiye anaupiga lakini kipa Cillessen wa Uholanzi anaudaka bila wasiwasi
23:10 Argentina 0-0 Uholanzi
23:09 Messi anapata FREEKICK ya kwanza kuelkea kwa Argentina
23:00 Mpira unaanza hapa sao Polo Argentina dhidi ya Uholanzi .
22:59 Perez amechukua nafasi iliyowachwa na Di Maria upande wa Argentina
22:59 Van Persiena De Jong wanaanza kwa upande wa Uholanzi
22:57 Wimbo wa taifa unachezwa hapa Sao Paolo
22:54Wachezaji wa Argentina Sergio Aguero na Marcos Rojo wamerejea
22:54 Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi atakabidhiwa majukumu mahsusi ya kuifikisha Argentina katika fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 1990.
22:53 Argentina wanatatizika kwa kumkosa mchezaji wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja
22:52 Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara mbili mfululizo .
22:50 Argentina inachuana na Uholanzi katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kombe la dunia Brazil
No comments
Post a Comment