Writen by
sadataley
5:42 PM
-
0
Comments
Fortaleza, Brazil. Mshambuliaji tegemeo wa Brazil, Neymar hatacheza tena Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo wakati waliposhinda 2-1 dhidi ya Colombia.
Neymar aligaragara chini kwa maumivu kabla ya
Marcelo kuwaita madaktari waliomtoa nje kwa machela na ku moja kwa moja
hospitalini.
Brazil pia itamkosa nahodha wake Thiago Silva
katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo
kupewa kadi ya pili ya njano. Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa
raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea
ushindi wa timu yao.
“Ni pigo kubwa kwetu,” alisema kiungo wa Brazil, Fernandinho.
“Tunahitaji kukaa pamoja na kushikamana baada ya
kumpoteza mchezaji wetu bora. Tutanyakua ubingwa wa Kombe la Dunia na
hiyo ndiyo itakuwa zawadi pekee kwa Neymar.”
Neymar ni mmoja wa nyota wakubwa kwa sasa Brazil,
pia katika mashindano hayo analinganishwa na mshambuliaji wa Argentina,
Lionel Messi. Sura yake imetawala katika mabango ya biashara barabarani
pamoja na televisheni.
Mashabiki wake zaidi ya milioni walitarajia
kumwona Neymar akimaliza Kombe la Dunia kwa kunyakua ubingwa, lakini si
kubebwa kwenye machela na kutolewa uwanjani.
“Neymar hahitaji kufanyiwa upasuaji,” alisema
daktari wa timu wa Brazil, Rodrigo Lasmar. “Lakini hataweza kucheza
mechi ya nusu fainali Jumanne dhidi ya Ujerumani.”
“Hatakuwa katika hali ya kuweza kucheza, anahitaji kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kurudi tena uwanjani,” alisema Lasmar.
“Amehuzunika sana kwa hali hiyo.”
Mashabiki 50 wa Brazil, wakiwa wamevalia jezi yake
ya timu ya taifa walikaa nje ya kliniki alipopelekwa Neymar, wakati
gari la wagonjwa likiwa limesimama kwenye mlango mkuu wa hospitali hiyo
bila ya kuzima taa zake.
Nyota wa dunia wamtakia pole Neymar
“Neymar, ni matumaini yangu utapona haraka rafiki
yangu!” - mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi aliandika
kwenye ukurasa wake wa Facebook.
‘Wote tupo nyuma yako @neymarjr! #ForcaNeymar’ - Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.
‘Nakutakia pole na upone haraka nyota, @neymarjr’ - beki wa zamani wa Brazil, Roberto Carlos.
‘Nimechukia kusikia taarifa mbaya ya Neymar!
Mchezaji wa kipekee. Nakutakia pole na upone haraka! #Ni mchezaji
kipenzi cha watoto wangu’ - aliandika nyota wa mpira wa kikapu, LeBron
James kutoka Miami Heat.
‘Nakutakia afya njema ndugu yangu. @neymarjr wote tupo nyuma yako, tunakupenda’ - kiungo wa Brazil na Chelsea, Willian.
‘Rafiki @Neymarjr, usife moyo, tunakuombea upone
haraka #forcaneymar’ - aliandika mchumba wake na mwanamitindo wa Brazil,
Gisele Bundchen.
‘Tuna furaha kwa ushindi, tunafurahi kucheza na
Brazil, habari mbaya kwangu ni @NeymarJr ni matumaini yangu utapona
haraka #ForcaNeymar #eTois #poldi #worldcup’ - mshambuliaji wa Arsenal,
Lukas Podolski, ambaye kikosi chake cha Ujerumani kitaivaa Brazil katika
nusu fainali.
‘@neymarjr ndugu yangu! nipo pamoja na wewe!’ - mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli.
No comments
Post a Comment