Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 24, 2014

HIVI UNAJUA MJI WA NINAWI UPO IRAKI? WAKRISTO WAPO KWENYE MATESO

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu, ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Mji wa Ninawi uonekanavyo kwasasa.
  Hii leo tumeamua kukujulisha moja ya mji ambao upo mpaka leo, habari zake zimeandikwa kwenye Biblia. Kama umesoma kitabu cha Yona katika Biblia utakutana na mji uitwao Ninawi ambao nabii Yona alitumwa na Mungu kwenda kuwahubiria habari njema lakini yeye akakwepa jukumu alilopewa na Mungu na kuamua kukimbilia Tarishishi, lakini kwakuwa Mungu hakimbiwi misukomisuko aliyoipata aliamua kujisalimisha kwa Mungu na kuitikia wito wa kwenda Ninawi kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Yona 3

Yona 3

1  Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,
2  Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.
3  Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.
4  Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.
5  Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
6  Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua
Ramani inayoonyesha mji wa Ninawi ulipo.
vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
7  Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
8  bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake.
9  Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
10  Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

  Mji wa Ninawi upo mashariki ya kati nchini Iraki. Mji huo unaoaminika kukaliwa na Wakristo wengi upo kilometa 400 kaskazini magharibi mwa Iraki, ingawa toka vita ilipoingia ya kumuondoa aliyekuwa Rais wa nchi ya Iraki marehemu Saddam Hussein, inaelezwa idadi ya Wakristo katika mji huo imepungua kwasababu baada ya mji mkuu wa Mosul kutekwa na waislamu wenye msimamo mkali wanaojiita Islamic state ama Isis zamani wakitambulika hivyo, kumewafanya wakristo wengi kuukimbia mji wa Mosul ambao majengo yake ni ya kisasa zaidi kulinganisha na Ninawi.


Watoto wakicheza nje ya nyumba zao huko Ninawi©nationalgeographical.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) katika taarifa yake ya habari hivi karibuni lilitangaza kwamba namba ya wakristo imeshuka kutoka milioni 1 na laki tano mwaka 2003 mpaka 350,000 - 450,000, ambapo wengi wao waliobakia wanaishi vijijini kama kijiji cha Qaraqosh ambacho pia kinafahamika kwa jina lingine kama Baghidada, Bartella, Al-Hamdaniya pamoja na Tel Kef ambavyo vipo ndani ya Ninawi.
Mwishoni mwa wiki iliyopita wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu)  na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji  ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka huu wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji. (Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).

Lango la kuingilia mji wa Ninawi lionekanavyo kwasasa©atlastours.
Habari kwa hisani ya Mtandao wa Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment