Writen by
sadataley
7:08 PM
-
0
Comments
|
Mtume Onesmo Ndegi, mwenyeji wa Kongamano hilo |
Zilikuwa ni siku sita za kwenda viwango vya juu katika Jiji la Dar es
salam Katika Kanisa la Living Waters Centre chini ya mtumishi wa Mungu
Mtume Onesmo Ndegi, kwenye 'Kongamano la Viwango vya Juu' (Higher Levels
Conference)
Kila mwaka kwenye Kanisa la Living Waters Centre huwa kuna Kongamano kuu
ambalo linakuwa na watumishi wa Mungu kutoka makanisa mbalimbali nchini
na nje ya nchi, ambapo kwa mwaka huu alikuwepo Askofu Kameta wa Dar es
salaam, Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Mchungaji Titus Mkama wa
Ilala TAG Dar es Salaam, Askofu Dkt Peter Muteba wa Afrika Kusini,
Askofu Dkt Tengu Yoka kutoka Nairobi, Mtume Aaron Timoth wa DRC, na
wenyeji Mtume Onesmo na Mwalimu Lilian Ndegi, ambapo watu walipata muda
wa kutosha kujifunza Neno la Mungu kwa ufasaha na kuombewa na watumishi
wote waliohudumu katika Kongamano hilo.
Living Waters Praise Team, Totoo, Kwaya kutoka Glory Land Arusha, na
kwaya kutoka Nairobi walipata kuhudumu kwenye kongamano hilo, huku pia
King Chavala akiwepo kufanya vitu vyake.
|
Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Gloryland International Church |
|
Mchungaji Titus Mkama wa Ilala
TAG Dar es Salaam |
|
Askofu Dkt. Peter Muteba, Afrika Kusini |
|
Askofu Dkt. Tengu Yoka kutoka Nairobi |
|
Living Waters Praise Team walipokuwa wakihudumu katika Kongamano hilo |
|
Askofu Dkt Peter Muteba na mkewe |
|
Mwalimu Lilian Ndegi |
|
Katika Siku ya mwisho ya Kongamano hilo kulikuwa na tendo la kumfanya
Askofu Dkt. Peter Muteba wa Afrika Kusini kuwa mzee wa heshima, pia
kuingia katika Agano na mtumishi huyo no na uhusiano wao katika Kanisa
la Living Waters Centre kama wanavyoonekana katika picha |
|
Askofu Dkt. Peter Muteba wa Afrika Kusini akipokea zawadi ya picha iliyochorwa kwa mkono |
|
Champagne kama ishara ya kujipongeza |
|
Totoo Mwanamziki Kutoka Afrika Kusini |
|
Watumishi
waliohudumu katika Kongamano hilo, kutoka kushoto ni Mtume Aaron Timoth
kutoka DRC, Askofu Dkt Tengu Yoka kutoka Nairobi Kenya, Askofu Dkt.
Peter Muteba - Afrika Kusini, Mwenyeji - Mtume Onesmo Ndegina Askofu
Oram Mustafa kutoka Arusha. |
|
Mwalimu Lilian Ndegi (kushoto) akiwa na baadhi ya wake wa watumishi walihudumu katika Kongamano hilo |
Habari na picha kwa hisani ya Tunu Bashemela.
Habari kwa hisani ya Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment