Writen by
sadataley
6:31 PM
-
0
Comments
Belo Horizonte, Brazil. Ujerumani inakutana na Brazil inayocheza kwa nguvu nyingi katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia, huku wenyeji hao wakipania kutwaa ubingwa kama zawadi kwa Neymar.
Kikosi cha kocha Joachim Loew, Ujerumani inahitaji
kufikia mafanikio ya 2002, ilipofanikiwa kucheza fainali dhidi ya
Brazil licha ya kuchapwa mabao 2-0, na sasa itakuwa katika mchezo
utakaopigwa mjini Belo Horizonte.
Brazil inalazimishwa kucheza kwa nguvu ikiwa bila
mchezeshaji wao, Neymar aliyeumia na nahodha wao, Thiago Silva mwenye
kadi mbili za njano, wakisaka nafasi ya kutwaa taji hilo nyumbani katika
Uwanja wa Maracana, Jumapili.
Taifa zima limeumizwa na kukosekana kwa Neymar
mwenye miaka 22, ambaye aliumia uti wa mgongo katika mchezo wa robo
fainali dhidi ya Colombia, lakini Ujerumani inatamani kama nyota huyo
angekuwapo.
“Siku zote inakuwa vizuri kama wapinzani wenu
wametimia, lakini hilo pia litaifanya Brazil iwe pamoja na watataka
kushinda kwa ajili yake (Neymar),” alisema kiungo wa Ujerumani, Bastian
Schweinsteiger.
Brazil walimchezea vibaya kiungo wa Colombia,
James Rodriguez, wakati Colombia walipokutana na Brazil kabla ya Juan
Zuniga kumgonga Neymar, tukio lilimfanya nyota huyo wa Selecao kupelekwa
haraka hospitali.
“Neymar ametufanya tuimarike. Ana uwezo wa kuuamua
mchezo wowote, hivyo kucheza bila yeye itakuwa ngumu,” alisema Willian,
winga wa Brazil.
“Tunajua ubora tulionao. Sote tuna huzuni ya
kumpoteza, lakini kwa sasa tuna nguvu zaidi kutokana na kile
kilichotokea na tuko tayari kutimiza ndoto zetu.”
Nyota huyo wa Chelsea mwenye miaka 25, Willian au
Bernard wanapewa nafasi ya kuanza katika nafasi ya Neymar wakati
watakapoivaa Ujerumani hii leo.
Schweinsteiger aliugusia mchezo huo akisema
mwamuzi anatakiwa kuwa makini zaidi juu ya mchezo wa Brazil, ambao
wamecheza faulo 59 katika michezo miwili iliyopita, ukilinganisha na 29
za Ujerumani katika michezo kama hiyo.
“Wabrazili kwa sasa si wachawi wa soka kama
walivyokuwa zamani, timu yao imebadilika sana na hata aina yao ya
uchezaji,” alisema Schweinsteiger.
“Rafu nzito kwa sasa ni sehemu ya soka yao, ni
jambo ambalo tunatakiwa kuwa nalo makini mno uwanjani, pia kwa mwamuzi,”
aliongeza.
No comments
Post a Comment