Writen by
sadataley
6:27 PM
-
0
Comments
Na MwananchiArusha. Watu nane wamejeruhiwa, mmoja kati yao vibaya baada ya watu wasiofahamika kurusha bomu katika mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine uliopo karibu na Mahakama Kuu jijini Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Issaya Mngulu
amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa
hakuna aliyepoteza maisha hadi sasa lakini majeruhi mmoja yuko mahututi.
“Hakuna aliyepoteza maisha lakini watu nane
wamejeruhiwa na mmoja hali yake ni mbaya, miongoni mwa majeruhi ni
watoto wawili wenye umri wa miaka 14 na 15” alisema Kamanda Mngulu.
Kwa mujibu wa Mngulu, madaktari katika hospitali
ya Rufaa ya Selian walikopelekwa majeruhi hao, wamekata mguu mmoja wapo
wa majeruhi baada ya kuona umeumia sana.
Mgahawa huo unatajwa kuwa ni maarufu jijini Arusha
na hutembelewa na raia wengi wakigeni japokuwa polisi haijaweza
kudhibitisha kama miongoni mwa majeruhi hao kuna raia wa kigeni.
Hadi sasa hakuna mtu au kikundi kilichotangaza
kuhusika na shambulio hilo lakini kamanda Mngulu alisema watu wawili
wameshakamatwa wakihusishwa na tukio hilo na kwamba wote ni raia wa
Tanzania.
Tukio hilo la bomu katika mgahawa huo ni
muendelezo wa matukio ya mabomu yanayoendelea kulikumba jiji la Arusha
ambapo mwezi Aprili mwaka huu watu wasiojulikana walirusha bomu katika
baa maarufu ya Arusha Night Park na kujeruhi watu kadhaa.
No comments
Post a Comment