Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 12, 2014

BRAZIL 2014: Ni Argentina na Ujerumani fainali


Wachezaji wa Argentina wakipongezana baada ya kufuzu kuingia fainali baada ya kuishinda Uholanzi kwa mikwaju ya penalti 4-2. Picha na AFP 
Na Mwandishi WetuSao Paulo, Brazil. Timu ya soka ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia baada kuitungua Uholanzi kwa mikwaju ya penalti 4-2, katika mchezo wa jana wa nusu fainali nchini Brazil.
Kipa wa Argentina, Romero, alikuwa shujaa katika mchezo huo baada ya kupangua penalti mbili na kuisaidia timu yake kutinga katika hatua ya fainali, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Corinthians mjini Sao Paulo.
Kwa matokeo hayo, Argentina sasa itavaana na Ujerumani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil jumapili katika Uwanja wa Maracana.
Uholanzi ilikuwa na mchezo wa kawaida tofauti na ilipocheza na Costa Rica katika hatua ya robo fainali, huku kasi ya Argentina ikionekana kubadilika kuliko ilivyokuwa katyika mchezo wao uliopita.
Nafasi chache katika mchezo huo zilishindwa kutumiwa vizuri na Arjen Robben, ambaye angeweza kuipa bao timu yakew dakika ya 90, lakini kiungo Javier Mascherano alimuwahi kabla ya kuleta madhara.
Mikwaju ya penalti iliyopigwa na Lionel Messi, Sergio Aguero, Ezequiel Garay na Maxi Rodriguez zilitosha kuipa ushindi Argentina huku Wesley Sneijder na Ron Vlaar wakikosa kwa upande wa Uholanzi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment