Writen by
sadataley
6:42 PM
-
0
Comments
Amesema kuwa ni vyema kwa viongozi hao kung’atuka
ili kutoa nafasi kwa vijana wenye nguvu na akili kulitumikia taifa
katika uongozi.
Warioba aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam
katika mahojiano maalumu na gazeti hili, pamoja na mambo mengine
alizungumzia uongozi wa nchi hii.
“Mwalimu Julius Nyerere aling’atuka akiwa na nguvu
zake kabisa. Kiasili kung’atuka ni dhana ya kuwapisha vijana kuwa mbele
katika kutekeleza majukumu na ninyi wazee siyo kuondoka, bali kuendelea
kuwapa ushauri na mwongozo,”alisema Jaji Warioba.
Alieleza kuwa kung’atuka kunamfanya aliyechukua
hatua hiyo kuishi maisha ya raha yenye furaha na amani jambo ambalo yeye
sasa analifurahia.
Aliongeza: “Haiwezekani mzee ukakaa kundi moja na
kijana wako aliyetahiriwa juzi, kwani kwa kawaida, kijana akitahiriwa
hupandishwa daraja na kukaa kundi la wakubwa, hapo wewe baba yake hata
kama una miaka 40, unahamishwa na kuingia kundi la wazee.”
Alifafanua kuwa hata katika uongozi ni muhimu
kung’atuka na kuwapisha vijana ili waweze kutumia akili na nguvu zao
kuendeleza taifa huku wakipata maelekezo na mwongozo kutoka kwa wazee.
“Maisha yangu sasa baada ya kuacha uongozi ni ya
furaha na amani bila woga kuliko wakati wowote, tofauti na nilipokuwa
bado kiongozi katika Serikali,” alisema.
“Ukiwa kiongozi unaweza kuishi kwa hofu na shaka
huku ukituhumiwa,” alibainisha Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu
na Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka 1985 - 1990.
Kauli ya Warioba imekuja huku kukiwa na kundi
kubwa la viongozi wenye umri mkubwa katika nafasi mbalimbali madarakani
muda mrefu, huku wakiendelea kutamani nafasi za juu zaidi. Miongoni mwa
viongozi hao, wapo wanaotajwa kuunda makundi ya kusaka urais wa Tanzania
katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Hii siyo mara ya kwanza viongozi wenye umri mkubwa kutakiwa kung’atuka madarakani.
Januari 14, 2010, Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
aliwashauri wazee watumie busara kupima uamuzi wa kugombea tena nafasi
za ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Pinda alitoa rai hiyo alipokuwa akijibu
maswali ya wahariri katika mkutano alioitisha kujibu maswali yao jijini
Dar es Salaam.
Kwa habari kwa kina ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Warioba-ataka-wazee-waondoke-madarakani/-/1597296/2339936/-/ijo5v0/-/index.html
Kwa habari kwa kina ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Warioba-ataka-wazee-waondoke-madarakani/-/1597296/2339936/-/ijo5v0/-/index.html
No comments
Post a Comment