Writen by
sadataley
6:38 PM
-
0
Comments
Jaji akiwa anamkabidhi Cristina nembo ya The Voice kwa ushindi wake. |
Baada ya kutangazwa mshindi kutokana na kura zilizopigwa huku asilimia 60 ya kura zote kwa upande wa simu akichaguliwa yeye, mtawa huyo aliwaongoza watu wote waliokuwepo katika fainali hizo kusema sala ya Bwana "Baba yetu uliye mbingun…. " kisha kutokwa na machozi ya furaha asiamini kilichotokea. Cristina ambaye inaelezwa anauwezo wa kuimba sauti za juu, katika fainali hizo aliimba wimbo wa What A Feeling kutoka katika filamu ya Flashdance.
Mtawa huyo amekaririwa akisema uwepo wake katika shindano hilo haukuwa kwaajili ya kuanza
Cristina Succia mwenye furaha. |
safari yake kimuziki bali kumtangaza Kristo na kuonyesha kipaji ambacho
amepewa na Mungu licha ya kwamba ni mtawa bado Mungu hakumpokonya kipawa
hicho. Cristina amesema kwamba maombi ni kipaumbele katika maisha yake
na kuamka mapema asubuhi na kwenda kufundisha shuleni kwake anakofanyia
kazi na kwamba hata kwenda kinyume na kiapo chake cha kazi na upendo
alionao juu ya muziki.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Italia zinasema uwepo wa Cristina katika shindano hilo ulimvutia hata Papa Francis na viongozi wengine wa Vatican ambao walikuwa wakimsikiliza mtawa huyo ambaye inaelezwa amejaaliwa sauti nzuri huku kadinali Gianfranco Ravasi akituma ujumbe wake kwenye mtandao wa twitter akisema "Tukiacha kutenda haki, Mungu atatupokonya muziki". Kwa ushindi huo mtawa Cristina ameingia mktaba na kampuni kubwa ya muziki ya Universal ambako atatoa album yake lakini pia anamkataba na shirika la utangazaji la Italia (RIA) huku pia akiwa bado mtumishi wa shirika la kitawa la Ursuline la nchini humo.
Cristina akiimba na mwanamuziki Kylie Minogue katika shindano hilo, Kylie alikuwa jaji wa The Voice UK mwaka huu. |
Hakika alidhamiria si unaona mwenyewe. Habari na Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment