Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, June 6, 2014

KINANA AITEKA MERERANI KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mererani wilaya ya Simanjiro ambao wengi ni wachimbajI wa wadogo wadogo wa madini kwenye mkutano wake mjini Mererani wilaya ya Simanjiro Manyara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mererani ambao aliwaambia vyama vya Upinzania ni sawa na Jogoo kwani hata awike vipi hawezi fungua mlango na kwa sababu vyama hivyo havipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi basi vinelekea kufa kwani havina sera mpya za kujinadi kwa wananchi.
 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Ndugu Christopher Ole Sendeka akihutubia wananchi wa Mererani wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM leo alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna wachimbaji wadogo wanavyotumia mashine kubebea mchanga kutoka kwenye mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM leo alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
 
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa madini wakiwa juu ya kifusi kushuhudia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi alioambatana nao wakiangalia mgodi unaomilikiwa na wachimbaji wa Kitanzania na ambao nyenzo zake za kufania kazi wamebuni wao wenyewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji litakaloweza kuhudumia watu 25,000 na kutoa  lita 36,000 kwa saa linalojengwa Naisinyai Mererani.
Mradi wa maji ukiwa kwenye hatua za mwisho mwisho Naisinayi Mererani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kuzindua tawi jipya la CCM tawi la Kandasikira.
 Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu akiwasalimu wakazi wa Kandasikira,baada ya tawi la jipya kuzinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM akikabidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM Bi. Upendo William baada ya kuzindua tawi jipya la CCM Kandasikira ambapo jumla ya wanachama wapya 153 walipewa kadi leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiangalia vikundi vya sanaa vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi katika kijiji cha  Landanai.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment