Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, June 6, 2014

ISRAEL HOUGHTON AHITIMISHA KILELE CHA MIAKA 30 YA WATOTO UGANDA KWA KISHINDO JANA

Israel Houghton akiimba nchini Uganda jana.
Hapo jana katika viwanja vya kanisa la Watoto Kyengera lililopo Kampala nchini Uganda, kulifanyika kilele cha maadhimisho ya miaka 30 tangu huduma ya Watoto kuanzishwa nchini Uganda, sherehe ambazo zilipewa jina la 'Watoto Big Party' zilipambwa na mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa injili duniani Israel Houghton na kundi lake la New Breed kutoka nchini Marekani.

Wageni wengine waliohudhuria kilele hicho ni pamoja na mchungaji kiongozi na mwanzilishi wa kanisa la Hillsong duniani lenye makao makuu yake nchini Australia Brian na mkewe Bobby Houston, wageni mbalimbali pamoja na watu waliolelewa na huduma hiyo toka ilipoanzishwa pamoja na waumini wa kanisa la Watoto ambalo limekuwa maarufu duniani kutokana na kwaya ya Watoto ambayo hufanya ziara kila mwaka duniani. Kusoma zaidi BONYEZA HAPA

Mambo yalikuwa safi, kuimba na kucheza.
Mwanadada Charlin Moore wa New Breed akisukuma sauti kumsifu Mungu.
Israel Houghton.
Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria hapo jana.
Waanzilishi wa huduma ya Watoto Gary na mkewe wakiwa wenye furaha.
Watoto Children kwaya wakimsifu Mungu.
Watoto Children kwaya wakiimba kwa furaha katika maadhimisho hayo.
Mmoja wa watoto akiimba kwa hisia, moja ya kisa ni kwamba baadhi ya watoto wanaoishi kijijini humo baadhi yao wazazi wao waliuwawa na baba ya watoto wengine ambao pia wapo kijijini hapo, ila watoto wote wamesameheana.
Vijana kutoka kanisa la Watoto wakiwajibika.
Brian Houston wa Hillsong na mkewe pamoja na waanzilishi wa huduma ya Watoto mchungaji Gary Skinner na mkewe.
Baadhi ya waimbaji waliokuwa upande wa kwaya kubwa.
Maelfu ya watu waliohudhuria usiku wa jana katika kilele hicho.

Kijiji cha Watoto ambacho kinatunza watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ukimwi na ambao walifariki kwa vita kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo jumla ya nyumba 406 mpaka sasa zimejengwa kwenye kijiji hicho. ©Watotochurch

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment