Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 11, 2014

RWANDA-UINGEREZA: Serikali ya Uingereza imesema yatiwa wasiwasi na wimbi la kukamatwa kwa watu raia nchini Rwanda RWANDA-UINGEREZA: Serikali ya Uingereza imesema yatiwa wasiwasi na wimbi la kukamatwa kwa watu raia nchini Rwanda


Rais wa Rwnda Paul Kagame mjini Davos, Jnuari 24, 2014.
Rais wa Rwnda Paul Kagame mjini Davos.

Na Ali Bilali
Serikali ya Uingereza imeeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Rwanda baada ya wimbi la kuwakamata raia wake kaskazini mwa nchi hiyo.


Kulingana na taarifa iliowasilishwa kwenye idhaa ya kifaransa ya RFI, imerejelea onyo lililotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ya hivi ya hivi karibuni kwa serikali hiyo.
Serikali ya Uingereza inakemea hatuwa ya kamata kamata hasa bila ya kuzingatia taratibu za msingi za kisheria, imesema taarifa hiyo, na kuongeza kuwa serikali ya Uingereza inafuatilia kwa karibu hali ilivyo nchini Rwanda na ambayo inawatia wasiwasi.
Juma hili, Balozi wa Uingereza nchini Rwanda amekutana na mtafiti wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch pia na Waziri wa Sheria wa Rwanda baada ya waziri huyo kulituhumu shirika hilo kuwa Msemaji kwa makundi ya kigaidi.
Aidha, serikali ya London imelaani mauaji ya Patrick Karegeya na mashambulizi dhidi ya makazi ya Kayumba Nyamwasa na wapinzani wawili wa serikali ya Rwanda wakiwa uhamishoni na kupongeza hatua ya uanzishwaji wa uchunguzi unaofanywa na polisi ya Afrika Kusini.
Msemaji huyo ameelezea wasiwasi wake kwa kile kinachoonekana kuwa ni mfululizo wa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya viongozi wa upinzani nchini Rwanda pamoja na kauli za baadhi ya viongozi wa juu wa serikali ya Kigali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment