Writen by
sadataley
5:53 PM
-
0
Comments
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.PICHA|MAKTABA
Na Daniel Mjema, Goodluck Eliona, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono wameingia
katika mvutano baada ya ujumbe wa maandishi wa kutaka kukwamisha bajeti
ya wizara hiyo kusambazwa kwa wabunge.
Habari za uhakika zilizopatikana jana zilieleza
kuwa kiini cha mgogoro huo ni ujumbe mfupi (SMS) ambao unamtuhumu Mkono
kula njama za kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Gazeti hili limedokezwa kuwa, SMS hiyo inadaiwa
kutumwa na Waziri Muhongo kwenda kwa baadhi ya wabunge akimtuhumu Mkono
kuwahonga baadhi ya wabunge Sh3 milioni kila mmoja ili kukwamisha bajeti
hiyo.
Ujumbe huo unasomeka ”Mhe Spika wa Bunge la
Jamhuri, Sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe Mkono ametufuata na
kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na
Madini.
Ujumbe huo umeanza pia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Jamii Forums .
Mkono
Mkono ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini,
alipoulizwa jana kama ni kweli amelalamika kwa Spika juu ya jambo hilo,
alikiri na kusema alichofanya ni kulalamika kwa Spika na amemwachia
alishughulikie.
“Ni kweli nimelalamika kwa Spika. Unajua taratibu
za Bunge ni kuna any complaint (lalamiko) unaliwasilisha officially
(rasmi) kwa Spika… hilo jambo lipo nimelifikisha kwa Spika wao ndiyo
watafuatilia kwa taratibu zao,”alisema.
Profesa Muhongo
Alipotafutwa kwa njia ya simu ili alitolee
ufafanuzi suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo alituma ujumbe kwa simu ukisema:
“Tutavuka tukiwa na ushindi wa maskini na wanyonge
wa nchini mwetu. Tutaendelea kujenga uchumi imara utakaotoa ajira mpya
na matumaini mapya kwa vijana, maskini na wanyonge wa nchini mwetu.
Watanzania wamechoshwa na wizi, udalali, ubabaishaji na rushwa.”
Mkurugenzi wa shughuli za Bunge, John Joel
alipotafutwa jana alisema yeye hana taarifa juu ya jambo hilo akisema
kama lipo, basi huenda likawa mikononi mwa Spika mwenyewe.
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Tuhuma-nzito-Bajeti-Nishati-na-Madini/-/1597296/2319024/-/m2kdf0z/-/index.html
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Tuhuma-nzito-Bajeti-Nishati-na-Madini/-/1597296/2319024/-/m2kdf0z/-/index.html
No comments
Post a Comment