Writen by
sadataley
5:49 PM
-
0
Comments
Moja kati ya mashambulizi ya kigaidi yaliyowahi kufanyika nchini Kenya
Balozi wa Marekani nchini Kenya,
Robert Godec, amesema kuwa uchunguzi wao umebaini Kenya ipo katika hali
ya hatari kubwa ya kushambuliwa na magaidi.
Bwana Godec ametaka usalama uimarishwe katika ubalozi wa Marekani nchini humo na maeneo mengine ya nchi.Bwana Godec amesema Marekani ipo tayari kufanya kazi na nchi ya Kenya kupiga vita ugaidi.
Taarifa hiyo ya balozi imetolewa baada ya kutokea milipuko miwili siku ya Ijumaa katika soko moja jijini Nairobi ambapo watu kumi na wawili walifariki dunia.
Tukio la kigaidi la mlipuko ndani gari lililotokea Nairobi miaka kadhaa iliyopita
Baadhi ya viongozi nchini kenya wametaka sheria ya ugaidi kurekebishwa ili washukiwa wa ugaidi wasiachiliwe kwa dhamana katika mahakama za nchi hiyo.
Pia wamelaumu hatua za mataifa ya magharibi zikiwemo Uingereza , Marekani na Australia kutoa tahadhari dhidi ya raia wao kwenda nchini Kenya.
Tayari mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa wamewasili mjini Mombasa wamerudi nyumbani baada ya onyo hilo kutoka kwa serikali yao.
Wizara inayosimaia utalii nchini Kenya inasema ina mpango wa kufufua sekta ya utalii kufuatia mashambulizi hayo ya kigaidi.
No comments
Post a Comment