Writen by
sadataley
4:27 PM
-
0
Comments
Mabaki ya kanisa la Sanjiang. ©The Telegraph |
Wakati hivi karibuni tumekufahamishwa namna gani makanisa yanafungwa na kuuzwa
nchini uingereza, huko China hali ni tofauti, kwani serikali ya nchi
hiyo imekuwa ikifanya juhudi ya kubomoa makanisa kila yanaposhamiri,
imefahamika.
Zoezi la ubomoaji likiendelea. ©International Christian Concern |
Tukio la hivi
karibuni ni kubomolewa kwa kanisa jipya lenye uwezo wa kuchukua watu
4000 walioketi, ambapo viongozi walitoa kisingizo kwamba msalaba
uliowekwa kwenye jengo la kanisa juu kwa nje, ulikuwa mkubwa sana na
wenye kuonekana kutokea mbali kiasi cha kuwafanya watu kushindwa kutilia
maanani kile wafanyacho.
Eneo ambalo linatambulika nchini humo
kwa kuyafanya maisha ya wakristo kuwa magumu kwa njkia hiyo ni jimbo la
Zhejiang, ambapo mnamo mwaka 2000 mamia ya makanisa na
majengo ya kuabudia wakristo yalivunjwa na uongozi wa mji huo.
Mwanzo wa tukio lenyewe inaelezwa kwamba ni pale katibu wa chama cha
Kikomunisti alipokuwa akifanya ziara kwenye mji wa Wenzhou na kisha
kuuona msalaba uliopo kwenye jengo la kanisa, ambapo aliagiza viongozi
walio chini yake kuwa uondolewe mara moja kwa kuwa ni mkubwa kupitiliza,
jambo ambalo viongozi waliokasimishwa jukumu hilo
waliamrisha kuwa msalaba na ghorofa la kwanza la kanisa hilo libomelewe.
Ujenzi wa kanisa hilo, enzi zake. Carlos Barri/Reuters |
Pamoja na kwamba hiyo ilikuwa ni amri ya serikali, maelfu ya wakristo
nchini humo waliungana kwa pamoja kuzuia jaribio hilo, na kufanikiwa kwa
siku kadhaa, ambapo serikali sasa ikatishia kubomoa jengo lote kabisa.
Lakini kama ambavyo husemwa mtaani kuwa, serikali ina mkono mrefu, mawasiliano ya eneo hilo yalidhibitiwa kiasi cha simu
kutofanya kazi na umeme kanisani hapo kuzimwa, na kisha polisi wa
kutuliza ghasia wakamwagwa eneo hilo kuwatawanya waumini, ili
kufanikisha tukio la ubomoaji wa kanisa hilo, kwa kutumia mabomu ya
kutegesha mishale ya saa mbili na nusu usiku siku ya Jumapili, na zoezi
hilo kuendelea Jumatatu.
Wakristo kutoka jimbo la Zhejiang wakiwa wanalinda lango kuu la kuingilia kanisani hapo. ©China Aid |
Maneno haya hapa kwetu yangekuwa yanasomeka kama "BOMOA". ©China Aid |
Kanisa hilo la Sanjiang limejengwa ka nguvu za familia zilizoungana
maeneo hayo, ambapo gharama yake imefikia kiasi cha dola milioni 4.8,
sawa na takribani shilingi bilioni 7.9 za Kitanzania, ambapo baadhi ya watu walijitolea kila walichokuwa nacho ili wapate
sehemu nzuri ya kumuabudu Mungu kwa amani na furaha.
Habari kwa hisani ya http://www.gospelkitaa.co.tz
No comments
Post a Comment