Writen by
sadataley
1:39 PM
-
0
Comments
Kate na Davie Oggs wakiwa na kichanga chao. ©Howlifebegan/youtube |
Hakuna furaha kubwa kwa mjamzito kujifungua salama, mtoto aliye na afya
njema. Na hakuna majonzi makuu kwa mjamzito kupoteza kichanga chake kwa
sababu yoyote ile, ikiwemo kuibiwa ama kufuariki.
Kilichotokea kwa mama huyu huko Sydney, (Autsralia) anayefahamika kwa
jina la Kate hakika hakielezeki kwa urahisi. Akiambatana na mume wake,
Daid Ogg - walifika hospitalini hapo ambapo mama huyo alijifungua watoto
mapacha kabla ya muda muafaka, ambapo walikaa tumboni kwa kipindi cha
miezi 6 tu.
Pacha wa kike, Emily alinusurika, wakati pacha wa kiume, Jamie,
alitangazwa na daktari kuwa amefariki punde tu baada ya kuzaliwa. Katika
hali ya majonzi, mama wa kichanga hicho, Kate - alishika mwili wa
kichanga chake hicho, huku akikiongelesha pamoja na mumewe licha ya
kwamba walishafahamishwa kuwa hauna uhai (a lifeless body) - kwa
kukitajia jina la dada yake, na kwamba anaendelea vizuri, huku pia
wakimuita kwa jina lake (japo hasikii)
Kwa masaa mawili wazazi hao waliuongelesha mwili wa kichanga hicho
ambacho hakikuwa na pumzi, na baada ya muda huo kila mtu akabaki ameduwa
baada ya kichanga hicho kufungua macho na kuungana na familia hiyo
ambayo ilijawa na furaha ya ajabu, ambapo wanaeleza tukio hilo kwamba si
kingine bali ni muujiza.
Hakika hapo pia tunakumbushwa kuwa maneno yana nguvu
ya kuumba ama kubomoa, jambo gani unalisema kwa mtoto wako ama mwenza
wako? Mjenge kwa namna ambavyo anatakiwa kuwa, ikiwemo kumpa jina zuri na sio kumsema kwa namna alivyo.
HABARI KWA HISANI YA Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment