Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, May 26, 2014

MASUALA YA KIROHO YALIVYOPENDEZESHA TANZANIA JANA

Hizi ni baadhi ya picha za matamasha yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam pamoja na Arusha, ambapo waimbaji mbalimbali walikuwa wakifanya matukio ya kumsifu Mungu ikiwemo kuzindua album zao pamoja na kurekodi.
1. Katika Kanisa la Kilutheri Mbagala jijini Dar es salaam kulifanyika uzinduzi wa album ya injili ya mwanadada Mercy Kitundu ambaye alisindikizwa na waimbaji mbalimbali kama Bahati Bukuku, Tumaini Njole, Christina Matai ambaye pia alikuwa msema chochote ama MC akishirikiana na Joshua Makondeko bila kumsahau Jerry Mtumishi. Mahudhurio ya watu yalikuwa mazuri sana sana.
Bahati Bukuku akimsifu Mungu jana KKKT Mbagala.
Christina Matai katika pozi na watumishi wenzake, Joshua Makondeko katikati.
Ilikuwa raha sana.
2.Hapo jana tena jijini Dar es salaam, kwaya ya The Reapers kutoka kimara KLPT walifanya live DVD rekodi yao ya kwanza kupitia kampuni ya AJM chini ya mkurugenzi wake mwanamama Joyce Mlabwa, tukio lilikuwa zuri na kazi njema ilifanyika katika kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) kwa mchungaji Huruma Nkone.
The Reapers kabla ya kupanda jukwaani.
Tukio likiendelea, mambo ya live hayo chini ya AJM Production.
The Reapers wakiwa jukwaani.
3. Kutoka kanisa la St. James Kaloleni Arusha, mmoja kati ya waimbaji nyota wa kwaya ya Tumaini Shangilieni, ambaye pia ni mwimbaji wa New life band ya jijini humo aitwaye Mathayo Lemabi, jana alitambulisha nyimbo zilizomo kwenye album yake mpya anayotarajia kuiweka wakfu wiki hii.
Matayo akimsifu Mungu.
Mungu amempa sauti kijana huyu, tafuta kanda za Tumaini, utakubaliana nami.
Baadhi ya wapigaji na waimbaji wa kwaya ya Tumaini Arusha wakifuatilia tukio kanisani kwao jana.
Upande mwingine pia waimbaji na wapigaji wa Upendo kwaya kwa mbali wakimsikiliza Matayo.
4. Huko mkoani Rukwa, kulikuwa na tendo la kusimikwa kwa askofu wa kanisa la Moravian mkoani humo aitwaye Conrad Ernest Nguvumali zilizofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo, pamoja na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Peter Mizengo Pinda.

Wachungaji na waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maandamano ya kusimikwa kwa askofu Nguvumali.
Kwaya ikimsifu Mungu.
Askofu Nguvumali akipeana mkono na waziri mkuu Mizengo Pinda. 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment