Writen by
sadataley
2:53 PM
-
0
Comments
Lilongwe, Malawi. Mahakama Kuu ya Malawi imepinga uamuzi wa Rais wa nchi hiyo, Joyce Banda kufuta matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) kwa madai kuwa hana mamlaka hayo.
Mahakama Kuu ilitoa uamuzi huo jana baada ya Rais
Banda kufuta uchaguzi huo kwa madai kuwa ulikuwa na kasoro, ikiwa ni
pamoja na vitendo vya wizi na matokeo kuchezewa kwenye kompyuta.
Wakati Rais Banda akitangaza kufuta matokeo ya
uchaguzi alisema: “Ninabatilisha matokeo ya uchaguzi kwa mamlaka
niliyopewa na katiba ya Malawi. Ninataka kuwapa Wamalawi nafasi nyingine
ya kuchangua mgombea anayefaa kwa uhuru.”
Aidha, Rais Banda alisema kuwa hatagombea tena
nafasi ya urais katika uchaguzi ambao alisema utafanyika ndani ya siku
90 kuanzia sasa.
Awali mawakili wa serikali ya Malawi, Kalekeni
Kaphale, Noel Chalamanda, Patrick Mpaka waliwasilisha pingamizi
mahakamani wakipinga Rais Banda kufuta matokeo hayo.
Chalamanda alisema mahakama hiyo imetupilia mbali
tangazo la Rais Banda kwa kuwa hana mamlaka ya kufuta matokeo ya
uchaguzi na kusimamisha kazi ya kuhesabu kura. “Mahakama imesema Rais
Banda hana mamlaka ya kufuta uchaguzi,” alisema Chalamanda.
Chalamanda alisema mahakama hiyo pia imeweka
pingamizi Rais Banda kutokana na hatua yake ya kufuta matokeo na
kusimamisha shughuli za kuhesabu kura.
Baada ya Rais Banda kutangaza kufuta matokeo, hali
ya wasiwasi ilitanda katika mji mdogo wa Limbe ambako polisi wa nchi
hiyo walikuwa wakipita huku na kule wakiwa kwenye magari.
Ulinzi uliimarishwa juzi katika mji huo baada ya
serikali kupata taarifa za kiintelejensia kwamba raia wa nchi hiyo
walipanga kufanya maandamano kupinga uamuzi wa rais huyo.
Kabla ya serikali kutuma polisi kwenye mji huo, wananchi walianzisha vurugu katika mji mkuu wa Blantyre.
Katika hatua nyingine, chama cha MCP kimetangaza
kwamba mgombea wake, Lazarus Chakwera ameshinda uchaguzi huo pia tume ya
uchaguzi na baadhi ya vyombo vimekuwa vikishambuliwa kwa kutangaza kuwa
mgombea wa Democratic Progressive Party (DPP) anaongoza kwa asilimia
42.
Kabla ya Rais Banda kutangaza kufuta matokeo hayo,
Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) ilitangaza matokeo ya awali ambayo
yalionyesha mgombea wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter
Mutharika alikuwa akiongoza kwa asilimia 42 baada ya kupata kura 683,621
akifuatiwa na Rais Banda ambaye alipata kura 372,101 sawa na asilimia
23 kupitia People’s Party (PP).
No comments
Post a Comment