Writen by
sadataley
2:52 PM
-
0
Comments
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dodoma. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewataja kwa majina mawaziri na wabunge aliosema bungeni kuwa wamekuwa ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na Mbunge wa Kongwa
ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi; Naibu Waziri wa Katiba
na Sheria, Angela Kairuki na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, Pindi Chana na wabunge Betty Machangu (Viti Maalumu),
Livingstone Lusinde (Mtera), John Komba (Mbinga Magharibi), Eugen
Mwaiposa (Ukonga) na Gudluck Ole Medeye (Arumeru Magharibi).
Hata hivyo, gazeti hili halijawataja majina
mawaziri na wabunge wengine waliomo kwenye orodha hiyo ya Lissu kwa kuwa
hawakupatikana jana kujibu tuhuma hizo.
Mbali na kuwataja kwa majina, Lissu pia ametoa
vielelezo vinavyoonyesha jinsi walivyokuwa wakiidhinishiwa malipo kwa
nyakati tofauti na Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za
Mitaa (LAPF), kwa sababu mbalimbali.
Lissu alimwambia mwandishi wetu jana kuwa licha ya
kiwango cha fedha kutokuwa kikubwa, lakini kinaweza kusababisha
mgongano wa kimasilahi kati ya wajibu wa wabunge kwa umma na masilahi
yao binafsi.
“Hali hii inaweza kusababisha Bunge likashindwa
kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuisimamia Serikali na taasisi
zake,” alisema Lissu huku akisisitiza azimio lake la kuwasilisha hoja
binafsi kwa Spika wa Bunge ili iundwe tume kuchunguza suala hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga jana alikiri
kuwa shirika hilo liliidhinisha malipo kwa mawaziri na wabunge hao kwa
ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Hata hivyo, alisema shirika hilo halitoi fedha
taslimu, bali hununua vitu ambavyo viliombwa na viongozi hao kwa ajili
ya kusaidia wananchi na si kufanya biashara.
Sakata lenyewe
Akizungumzia jinsi mawaziri na wabunge hao
walivyosaidiwa, Lissu alisema LAPF ilitoa Sh2.5 milioni kwa ajili ya
mradi wa madarasa Jimbo la Kongwa linaloongozwa na Ndugai.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Ndugai alisema hakuna tatizo lolote kwa mbunge kupewa msaada na mfuko wa kijamii.
“Huyo Lissu ana upungufu mkubwa. Hivi LAPF
ikisaidia Sh2 milioni kwa ujenzi wa darasa unaogharimu Sh10 milioni ni
tatizo hilo? Nchi hii inakwenda wapi jamani, siyo kila kitu
wanachozungumza wapinzani ni hoja, kama LAPF wangekuwa wanatoa fedha
lingekuwa tatizo lakini wanasaidia vifaa tu.”
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/wabunge-waomba-fedha-watajwa/-/1597296/2326624/-/e17j04/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/wabunge-waomba-fedha-watajwa/-/1597296/2326624/-/e17j04/-/index.html
No comments
Post a Comment