Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 6, 2014

Kiir yuko tayari kuzungumza na Machar kuleta amani Sudan Kusini


Rais Uhuru Kenyatta akimkaribisha Rais Salva Kiir State House Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta akimkaribisha Rais Salva Kiir State House Nairobi. 
 
Rais Salva kiir wa Sudan Kuisni amesema yuko tayari kukutana na makamu wake wa zamani ambae sasa ni kiongozi wa uwasi Riek Machar katika kujudi za kutafuta amani na kusitisha mapigano nchi ni mwake.

Kufuatana na msemaji wa afisi ya rais wa Kenya, Rais Kiir aliwambia marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda mjini Nairobi jana usiku kwamba atakuwa na mazungumzo ya amani na mhasimu wake mkuu.

Rais Kir alikwenda Nairobi siku ya Ijuma kwa mkutano wa kikanda juu ya miundo mbinu, kuhusu miradi ya ujenzi wa barabara kuanzia Juba hadi lamu na barabara kuu kutokea Mombasa hadi Bujumbura.

Kiongozi huyo wa Sudan Kusini alikutana na rais Kenyatta Jumamosi asubuhi na kumeleza juu ya mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry mjini Juba siku ya Ijuma.

Rais Kenyatta, anaeongoza Jumuia ya Ushirikiano wa Serikali ya Afrika Mashariki na Pembe mwa Afrika IGAD, kwa wakati huu, alieleza wazi kwamba Jumuia hiyo haitokubali kuvunjika vunjika kwa mazungumzo yanayoendelea ya kutafuta amani kwa wakati huu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment