Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 6, 2014

Al-Sisi atarajiwa kushinda urais Misri

Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Hamdeen Sabahi ndiye anayeshindana na al-Sisi katika kinyang'anyiro cha urais nchini Misri
Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Hamdeen Sabahi ndiye anayeshindana na al-Sisi katika kinyang'anyiro cha urais nchini Misri
 
Mkuu wa zamani  wa majeshi nchini Misri, Abdel Fattah  al Sisi, ambaye alimuondoa madarakani rais kutoka chama cha Ki-Islam, Mohamed Mursi, anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais mwezi huu na alisema kulikuwepo na majaribio mawili ya kutaka kumuuwa.

Al sisi alisema katika mahojiano ya pamoja na vituo viwili binafsi vya televisheni nchini  Misri, cha CBS na ONTV  kwamba “kulikuwepo na majaribio mawili ya kuniua . Nina muamini mungu,  siogopi”.

Hakusema ni lini majaribio hayo ya kutaka kumuuwa yalitendeka. Al Sisi anatarajiwa kushinda kiurahisi kwenye uchaguzi wa rais wa Mei 26 hadi 27. Mgombea pekee anayeshindana naye ni mwanasiasa mmoja kutoka mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabahi, ambaye alikuwa wa tatu katika uchaguzi wa mwaka 2012 ambapo Mursi alipata ushindi.

Tangu jeshi lilipomuondoa madarakani Mursi mwezi Julai mwaka jana, wanamgambo wameuwa mamia kadhaa ya wanajeshi wa  usalama katika mashambulizi ya mabomu na ufyatuaji risasi. Waziri wa mambo ya ndani nchini Misri alinusurika jaribio moja la kuuwawa mwezi Septemba.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment