Writen by
sadataley
3:21 PM
-
0
Comments
Mchungaji Joel Osteen, kiongozi wa kanisa la Lakewood la nchini Marekani. |
Kanisa hilo limetaka mtu yeyote aliyehudhuria ibada kanisa hapo siku ya jumapili awe makini na akaunti yake ya benki na endapo atagundua jambo lolote lenya ualakini katika akaunti yake basi atoe taarifa haraka iwezekanavyo. Kanisa hilo limewatoa wasiwasi waumini wake kwamba kitendo hicho kisitafsiriwe kwamba kanisa linavujisha taarifa zao bali sadaka hizo zilikuwa za mchango maalumu uliokusanywa wiki iliyopita.
"Tunafanya kazi na polisi kwa ukaribu kushughulikia tukio lililojitokeza", taarifa ya kanisa ikiwa imenukuliwa hivyo, mchango huo tayari ulikuwa una bima hivyo wanaangalia utaratibu na kampuni ya bima ili warudishiwe fedha zilizoibiwa kwa kanisa. Mchungaji Joel ni kati ya wachungaji ambao wanapitia majaribu ya kusemwa vibaya ikiwa pamoja na watumishi wenzie huku pia akihusishwa kuabudu vitu tofauti na Mungu, kubwa zaidi inadaiwa huwa ataji Yesu mara nyingi kwenye mafundisho yake. Lakini licha ya hayo yote huduma yake imekuwa ikihudhuriwa na watu takribani 45, 000 kila wiki.
Sehemu ya kanisa la Lakewood linavyoonekana kwa ndani, Joel akiwa madhabahuni akifundisha.©Lakewood church. Chanzo : Charisma. Habari kwa hisani ya Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment