Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 16, 2014

CHAGUO LA GK BAADA YA BARNABA NA AMBWENE, SASA NI AMINI, THT NA EPHRAIM SEKELETI.


Kutoka kushoto ni Ephraim, Silas Mbise pamoja na Sipho Makhabane wa Afrika ya kusini, wakiwa studio za WAPO Radio Fm, mwaka jana.
Habari za jumapili msomaji wa GK, karibu katika chaguo letu la jumapili, ambapo kama ilivyokuwa kwa wiki iliyopita tulipokuchagulia wimbo wa Upendo ulioimbwa na Ambwene Mwasongwe kisha kijana Barnaba Elias wa kundi la THT kuuimba wimbo huo kwa ustadi.

Leo tena tunakuletea wimbo uitwao Uniongoze ulioimbwa na mwanakaka Ephraim Sekeleti wa Mutalange kutoka pale nchini Zambia, wimbo huu umeimbwa tena na vijana wa kundi la Tanzania House of Talents (THT) ukiongozwa na Amini, wimbo huu waliuimba wakiwa katika ziara nchini Marekani, ambapo wameuimba bila vyombo na kwa ustadi mzuri.

Pamoja na wimbo huo, pia mtazame Ephraim Sekeleti akiwa katika kanisa la Living water Makuti Kawe, ambapo aliimba wimbo huo akitangulia na wimbo wake mpya usemao wewe ni Bwana usiyelala. Tunakutakia baraka za Mungu utazamapo nyimbo hizi, lakini pia wakumbuke vijana hawa ambao inaonyesha wanasikiliza nyimbo za injili basi wasiishie kuziimba tu bali pia wapate kumjua Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Linah na Amini wa kundi la THT wakiwa katika pozi..
          Mcheki Ephraim akiimba live katika moja ya ibada kanisa la Living water Makuti Kawe.
                                                                              Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment