Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 13, 2014

Papa Francis na uongozi wa kipekee

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.PICHA|MAKTABA 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ametimiza mwaka mmoja tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo.
Katika miezi yake 12 ya uongozi, Papa Francis amefanya mambo kadhaa muhimu ambayo watangulizi wake walishindwa kuyafanya, huku akitoa kipaumbele katika ujenzi wa kanisa hilo katika maeneo yenye ongezeko kubwa la watu na kuwajali masikini.
Papa Francis aliingia madarakani Machi 13, 2013 na kupewa nafasi ya kuliongoza kanisa hilo lenye zaidi ya waumini bilioni 1.2 duniani.
Miongoni mwa mambo yasiyo ya kawaida aliyofanya baada ya kuchaguliwa, ni pamoja na kukataa kutumia gari maalumu kwa ajili yake.
Gari hilo lilikuwa limefunikwa kwa kioo, hivyo kukiuka utaratibu wa awali uliowekwa na Kanisa wa kuwalinda viongozi wao wakuu baada ya Papa John Paul II kupigwa risasi.
Pia Papa Francis aliwahi kusafiri katika basi moja na makadinali. Kama haitoshi, pia alikataa kutumia gari aina ya Mercedes, badala yake alitumia gari aina ya Renault iliyokuwa na miaka 20, huku ikiwa imetembea zaidi ya kilomita laki mbili.
Akielezea aina ya uongozi wake, mwandishi Chris Boeskool anasema uamuzi huo siyo tu ni wa hatari kwa usalama, bali unaonyesha ni namna gani asivyojali kuhusu kifo.
Pia, Papa Francis anaamini kuwa kufanya jambo zuri ni bora kuliko kuamini jambo hilo na kuishia kulisema tu.
“Bwana ametukomboa sisi sote, siyo Wakatoliki peke yao wanaoamini kuwapo kwa Mungu na wasioamini,” aliwahi kusema.
Pamoja na umri wake mkubwa, Papa Francis amekuwa mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii. Kwa mfano, akaunti yake ya mtandao wa Twitter ina watu zaidi ya milioni tatu wanaomfuatilia duniani kote.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment