Writen by
sadataley
11:25 AM
-
0
Comments
Askofu mkuu wa kanisa Anglikana Uganda Stanley Ntagali akizungumza na vyombo vya habari nchini humo.©changing attitude |
Akizungumza na mwandishi wa AFP askofu mkuu wa kanisa hilo ambalo
linaheshima na wafuasi wengi nchini Uganda Stanley Ntagali, amesema nchi
za magharibi zinapaswa kuheshimu msimamo na sheria za nchi ya Uganda
dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja kama hawataki kuheshimu hilo wao
kama kanisa Anglikana nchini humo wako tayari kujitoa kwenye muungano
wa makanisa hayo na kujiendesha lenyewe.
Askofu Ntagali amesema vitendo vya kishoga ni kinyume na neno la Mungu
na kwamba hakuna kiongozi wa kweli wa kanisa ambaye ataruhusu vitendo
hivyo ikiwa na kuruhusu watu hao kuoana na kupata kibali cha ndoa na
kuongeza kwamba wakiwa katika muunganiko wa kanisa la England
wasingependa kuona kanisa hilo linaruhusu vitendo hivyo endapo
wataruhusu wao kama kanisa nchini Uganda watajiondoa.
Askofu Stanley Ntagali katikati na wasaidizi wake wakiwa katika moja ya huduma nchini humo ©Church of Uganda. |
Tangu Rais Yoweri Museveni apitishe sheria hiyo ya watu wanaojihusisha
na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupata kifungo cha maisha
gerezani, sheria hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti katika nchi
mbalimbali duniani hususani nchi za magharibi ambako vitendo hivyo
vinaruhusiwa kwa asilimia kubwa hadi mataifa hayo kufikia hatua ya
kumtaka Rais Museveni kutengua sheria hiyo kwakuwa inakwenda kinyume na
haki za binadamu. Rais Museveni alikaririrwa katika moja ya mahojiano
akisema "hakuna uthibitisho wa kusema mtu anaweza kuzaliwa shoga…. na
mwanaume kumpenda mwanaume mwenzake wakati kuna wanawake wengi warembo
wamejaa.. ni uchaguzi wa mtu na si vinginevyo, baada ya kuwasikiliza
wana sayansi nimegundua nimepata ukweli" alikaririwa Rais Museveni.
Ukiachana na mataifa ya magharibi ambayo yameijia juu Uganda kwa msimamo
wake huo, lakini tukio lililowashangaza waumini wa dini ya Kikristo
waliowengi Afrika ni kitendo cha askofu mkuu mstaafu wa kanisa hilo
nchini Afrika ya kusini Desmond Tutu naye amelaani Uganda kupitisha
sheria hiyo huku pia kukiwa na fununu kwamba askofu huyo aliyeonyesha
wazi kuunga mkono vitendo vya mapenzi ya jinsia moja yuko njiani
kuanzisha chama kitakachounga vitendo hivyo.
Kanisa kuu la Anglikana Mtakatifu Paul Kampala nchini Uganda. ©Church of Uganda Habari na Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment