Writen by
sadataley
11:27 AM
-
0
Comments
IDUMU INJILI MTAANI, DODOMA KITAELEWEKA TU
Mara zote inaia moyo kuona kwamba bado kuna huduma ya Injili mtaani, na
kwamba wako wenye kuitwa kwa namna hiyo wapate kupanda mbegu na kisha
kusubiria mavuno. Hali ndivyo ilivyo kwa Bwana Oscar Mwanyanje, mhitimu
wa shahada ya uhasibu kutoka chuo cha biashara (CBE) Dodoma.
GK ilipomtia machoni, ilipata shauku ya kujua kunani, ili basi nawe
upate kujuzwa mwanzo wa jambo hili ukoje. Kwa maelezo ya Bwana
Mwanyanje, anasema kuwa ameitiwa kwa hili jambo, na punde tu alipohitimu
masomo mwaka jana, basi sauti ya kuhubiri Injili mtaani ilimjia.
Hakuna kulala hadi kieleweke, wiki ya pili ya injili inasonga. |
Licha ya kwamba alijua kwamba ndani yake jambo hili limekuwepo kwa muda
mrefu, aliufanya moyo kuwa mgumu kutii, jambo ambalo anasema lilimletea
matatizo makubwa hata kiasi cha kukaribia kufa.
Muuzaji wa Biblia pamoja na wapita njia wengine wakimshangaa Oscar Mwanyanje wakati akihubiri maeneo ya uhindini, Dodoma. |
Kwa elimu yake, na kwa baadhi ya kazi ambazo aliwahi kuomba, anaeleza
kwamba zingine zilikuwa rahisi, na hata 'interview' kuwa rahisi, lakini
kuna siku alipotoka kwenye 'interview', sauti ikamjia ikimwambia kuwa
hatopata kazi hadi afanye kwanza kile ambacho Mungu amemuagiza.
Halikadhalika, Bwana Mwanyanje ametoa rai kwa wajumbe wa bunge maalumu
la katiba kumtafuta Mungu kwanza, kwani kutokana na ukinzani wa mawazo
kutoka makundi mbalimbali ya wajumbe hao bungeni, hawatoweza kufikia
muafaka kwa maslahi ya taifa, basi ni vema wakatambua kwamba Bunge
linamhitaji Mungu.
Huyu hapa mtaani, na biashara ya Mungu, akisubiri mavuno apatae kupanda
ngazi zaidi. Nini kulichopo mbele yake kwa mtumishi huyu anayelelewa na
Mchungaji Vangaste wa kanisa la Pendo Revival Center lililoko Area D
mjini hapo? Tusubiri na kuona, huku tukiombea Injili mtaani isikome kwa
manufaa ya Kristo. Mtumishi huyu anapatikana kwa namba za simu,
0752473707 na 0713312797
Oscar akiishia na megaphone yake kuelekea sokoni akapate kuhubiri zaidi injili ya wokovu. |
No comments
Post a Comment