Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 15, 2014

Njama ya Nazi kuua watu kwa Malaria

Vimelea vya Malaria
Mwanabayologia mmoja nchini Ujerumani amesema kuwa amepata ushahidi kuwa utawala wa Nazi uliokuwa unaongozwa na Adolf Hitler, ulikuwa unalenga kutumia Mbu kama silaha wakati wa vita vya pili vya dunia.
Klaus Reinhardt kutoka chuo kikuu cha übingen, alichunguza kumbukumbu za kitengo cha utafiti kilichokuwa katika kambi moja ya mauaji ya Dacahu mwaka 1944.
Reinhardt anasema kuwa wanasayansi walikuwa wanajaribu kupata Mbu ambaye angeambukizwa vimelea vya Malaria na kuwaeneza katika maeneo ya maadui kwa wingi ili waweze kuwaambukiza watu wengi iwezavyoAnasema aligundua kuwa amri hiyo ilitolewa na mkuu wa kitengo cha jeshi, Heinrich Himmler.
Inajulikana kuwa wafungwa waliokuwa wanusbiri kuuawa katika kambi hiyo waliambukizwa ugonjwa wa Malaria.
Duru zinasema kuwa mipango hiyo haikufanikiwa kwa sababu wajerumani walikuwa wanashambuliwa vikali wakati huo wa vita.
Chanzo: bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment