Writen by
sadataley
10:03 AM
-
0
Comments
Umoja wa mataifa unataraji kuwafikishia chakula na dawa raia waliokwama katika mji Homs kufuatia vita vikali kati ya waasi na vikosi vya serikali.
Siku ya ijumaa zaidi ya watu 80 waliondolewa katika maeneo ya waasi ambayo yamezingirwa kwa takriban mwaka mmoja na nusu sasa.Msafara wa misaada hiyo unatarajiwa kuingia katika mji huo ikiwa ni siku ya pili ya makubaliano ya mda ya kusitisha vita kati ya serikali na waasi.
Wengi ya wanaoondoshwa katika eneo hilo wameonekana wasio na nguvu na waliochoka.
Baadhi yao wamesema kuwa hawajala mkate kwa tarkiban miezi mitano sasa.
Chanzo: bbc swahili
No comments
Post a Comment