Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 8, 2014

ICC kuchunguza uhalifu wa kivita CAR

Waisilamu wamekuwa wakishambuliwa nchini CAR na sasa wameanza kutoroka
Mwendesha mkuu wa mashitaka katika Mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, Fatou Bensouda, ameanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Fatou Bensouda amesema kuwa amepokea ripoti za ukatili kutendewa makundi kadhaa yanayohusika na vita nchini humo.
CAR, ambayo ni moja ya mataifa masikini sana barani Afrika, imekuwa ikikumbwa na vurugu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa baada ya waasi waisilamu kuingia mamlakani kimabavu.Maelfu ya waisilamu tayari wameanza kutorokea nchini Cameroon na Chad.
Bensouda alisema kuwa uchunguzi wake unahusu mauaji ya mamia ya watu, visa vya ubakaji na utumwa wa kingono , uharibifu wa mali uporaji, mateso, kuhamisha watu kwa nguvu na kutumia watoto kama wapiganaji.

Aliongeza kuwa katika matukio mengi, waathiriwa wameonekana kulengwa kwa misingi ya dini.

Ghasia nchini CAR zinaonekana kuchukua mkondo wa ukatili huku kukiwa na taarifa za makundi ya watu kuwaua wengine hadharani .
Mnamo siku ya Ijumaa asubuhi, maelfu ya waisilamu waliripotiwa kutoroka wakiwa wameabiri malori mjini Bangui kutafuta usalama katika mataifa jirani. Walisaidiwa na wanajeshi wa kulinda amani wa Chad.
Mmoja wa watu hao aliyeanguka kutoka kwenye lori aliuawa na umati wa watu huku mwili wake ukikatwa katwa.
Kiongozi wa waasi, Michel Djotodia, aliyeingia mamlakani kimabavu, alijiuzulu mwezi jana kama sehemu ya mkakati wa kuleta amani nchini humo lakini ghasia zimeendelea tangu hapo.
Chanzo: bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment