Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 6, 2014

Kanisa katoliki imiikosoa vikali ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu tuhuma dhidi Maaskofu na mapadri


Viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki, mjini Vaticani
Viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki, mjini Vaticani

Na RFI
Uongozi wa kanisa katoliki duniani mjini Vatican umelaani vikali ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hapo jana ikilituhumu kanisa hilo kuwalinda mapadri na maaskofu ambao wanatuhumiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto.

Punde mara baada ya kutolewa kwa ripoti ya UN inayokemea sera za kanisa hilo pamoja na viongozi hao wa kidini kulindwa na uongozi wa juu wa kamati ya Papa, bado kanisa hilo limedai ripoti hiyo ni ya uongo na inayopandikiza chuki kwa waumini wake kwa kuwa kwa sehemu kubwa imetekeleza mapendekezo mengi ambayo yametolewa na tume ya Umoja wa mataifa iliyokuwa ikichunguza tuhuma za udhalilishaji wa watoto dhidi ya kanisa hilo.
Wakati wamahojiano yao na kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa majuma kadhaa yaliyopita, viongozi wa kanisa hilo walikiri kuwepo kwa vitendo hivyo na kwamba kesi nyingi wamezishughulikia kama kanisa na ni masuala yanayohusu imani zaidi.
Ripoti ya UN inalitaka kanisa hilo kuwakabidhi mapadri na maaskofu waliohusika na vitendo hivyo kwa vyombo vya usalama, pamoja na kuondoa ukiritimba wa upatikanaji wa taarifa muhimu za ndani ya kanisa hilo kuhusu matukio kama haya.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment