Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 15, 2014

Zoezi la kupiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya nchini Misri linaendelea

Raia nchini Misri wakipiga kura ya maoni

Na RFI
Wananchi wa Misri wanapiga kura ya maoni ya katiba ya nchi hiyo kwa siku ya pili mfululizo hii leo ambapo wito umetolewa na viongozi wa kijeshi nchini humo kupiga kura ya ndio ya katiba hiyo, na wengi wa wanaopiga kura katiba hiyo wanapiga kura ya ndio.

Juma moja kabla ya uchaguzi huo vyombo vya habari vimekuwa vikwatolea wito wananchi kupiga kura ya ndio badala ya kuipinga na ambapo wanasema kuipinga ni kuunga mkono ugaidi.
Wakati wa kampeni, wanaharakati 7 walitiwa nguvuni kwa tuhuma za kupiga kampeni kwa wananchi kuipinga katiba hiyo.
Licha ya hayo yote, hayakuzuia wananchi kupiga kura ya hapana.
Katiba hiyo mpya iliondaliwa na watu walioteuliwa na kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sissi, na iwapo itaidhinishwa basi itampa madaraka zaidi kiongozi huyo wa kieshi ambaye tayari ameonyesha nia yake ya kuwania uchaguzi wa rais.
Katiba hio mpy iliandaliwa, baada ya aliekua rais wa nchi hio Mohamed Morsi kuwekwa jela kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, na anakabiliwa kifungu cha maisha jela.
Jenerali Abdel Fattah al-Sissi anatuhumiwa na wafuasi wa aliekua rais wa nchi hio Morsi kuhusika na mapinduzi ya serikali yake.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment