Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Thursday, December 12, 2013

Wanamichezo wamkumbuka Mandela

Wanamichezo mashuhuri, duniani wametoa rambi rambi zao kwa hayati Nelson Mandela, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Wanamichezo pia wamemkumbuka Mandela
Muhammad Ali alisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Mwanasoka mashuhuri BofyaPele naye amesema "Mandela alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana maishani mwake. Ni shujaa wangu.’’
Mwanamasumbwi BofyaAli aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.
Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''
"BofyaAli amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.’’
BofyaTiger Woods, naye ambaye ni mchezaji golfu mashuhuri zaidi duniani, alisema daima atamkumbuka Mandela.
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza, BofyaDavid Beckham alisema kuwa anamlilia sana Mandela na kuwa yuko pamoja na familia yake. ''Tumepoteza mtu muhimu sana na shujaa wetu,’’ Alisema Beckham.
Naye mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, BofyaSepp Blatter, amesema kuwa anaomboleza sana na anahisi uchungu mwingi kufuatia kifo cha Mandela.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment