Writen by
sadataley
10:52 AM
-
0
Comments
Mwigizaji na mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka Ja Rule wa nchini Marekani ameweka bayana namna alivyompokea Yesu, wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Huff post live, ambapo ameweka bayana kwamba aliokoka katika kanisa la Hillsong New york ambako amesema wanapokea mtu jinsi alivyo bila kumuhukumu, akieleza zaidi Ja Rule ambaye jina lake kamili ni Jeffrey Atkins amesema alishangaa kuona kanisa ndani ya Club(ni kawaida ya Hillsong kukodi kumbi kubwa na kufanya ibada siku za jumapili) kukiwa na mataa kama ya disko, zaidi alishangazwa kuona mchungaji kavaa suruali ya jeans pamoja na fulana hali iliyomfanya kujisikia karibu zaidi na hatimaye kuokoka.
Mwigizaji huyo ameigiza filamu mpya ya Kikristo ambayo kuna mkono wa askofu T.D Jakes iitwayo "I'm in Love with A church Girl" filamu ambayo ndio iliyompelekea mwimbaji huyo kujikuta Hillsong na kuokoka, awali mwimbaji huyo alikuwa muumini wa kanisa la Mashahidi wa Jehova ama waite Jehova witness, ambapo kwasasa kanisa lake ni Hillsong New York, na jumapili ya jana kanisa hilo limefungua tawi katika mji wa Los Angeles ambako inaaminika itawavuta waimbaji na waigizaji wengi zaidi kwa Yesu.
No comments
Post a Comment