Writen by
sadataley
11:09 AM
-
0
Comments
Ufuatao ni ufafanuzi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God kupitia askofu wake mkuu, Barnabas Mtokambali, kutokana na sintofahamu kuhusiana na mahala alipozikwa Askofu Moses Kulola, ufafanuzi huu ulitolewa tarehe 4 Septemba, ambapo Askofu Mtokambali ameeleza kuwa walichofanya ni kuweka records sawa ili huko mbeleni maafa yasije kujitokeza.
Zifuatazo ni sehemu ya nukuu alizozungumza askofu Mtokambali, unaweza pia kuisikiliza sauti yake kama ambavyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, ripoti ya Yaliyotokea, kipindi cha WAPO Radio FM imenukuliwa.
Mila za kiafrika mtu akizikwa pale, pale panakuwa pake. Sasa tukasema kama tukikaa kimya, hili likatokea, baadae huko mbele tutasema nini, tutajibu nini kwasababu kanisa sio langu, kanisa ni la general council, mimi nawajibika kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, kwa wachungaji wote, halafu sisi tutaondoka watakuja watoto hapa, wanataka kuchukua kanisa lao na kuna kaburi pale, wasije watu wakachinjana hapo, tupate muongozo wa kisheria, ndio hilo tu, muongozo wa kisheria juu ya jambo hili jamani isije ikatokea confusion huko mbele, lakini niwaambieni ukweli, hakuna mtu aliyefurahi kama mimi mzee Kulola kuzikwa Bugando, mimi nimefurahi saana naomba muandike, nimefurahi saana Mzee Kulola kuzikwa Tanzania Assemblies of God Bugando.
...Sasa Mzee, kwa heshima zote ameanza kazi Tanzania Assemblies of God, mwaka 68, na Mzee ameombwa na EAGT, uongozi kwa busara yao kubwa na nzuri wameona alipoanzia ndio apumzishwe, amerudishwa nyumbani – amerudishwa nyumbani baba yetu, hakukuwepo na sababu yaani mimi kama TAG, na kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, lengo letu ilikuwa ni kuweka tu record sawasawa, kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo kuzuia maafa makubwa yanayoweza kutokea baadae, lakini kamwe haikuwa hasa kuzuia, mzee azikwe pale.
Hata kesho tutakaporudishiwa lile jingo lile, tutakaporudishiwa pale mahali kumiliki asilimia 100, mtu akitaka kuja kumuondoa pale mzee nyumbani, mimi nitaweka stop order usimuondoe, utamuondoa umpeleke wapi, na mzee amelala nyumbani, nitasema jamani hapana mwacheni mzee amelala nyumbani.
Sisi tumetumia uungwana sana na uvumilivu wa hali ya juu sana, na kama kweli watu wangekuwa wanataka kuandika watu ambao kweli ni wakristo, na wameonyesha uvumilivu, tolerance ni sisi. Ni pamoja na kanisa la Temeke, ndio maana unaona pale hakuna development inayofanyika, wanajua sio petu, angalia makanisa mengine ya EAGT yanavyoendelezwa, nenda Temeke hamna kitu, hata Bugando hakuna kitu kilichoendelezwa pale, maana na wenyewe wanafahamu.
Kwa hiyo tumekuwa wavumilivu sana na tumekuwa waungwana sana, tukitarajia wenzetu.. unajua Biblia inasema mwana mpotevu akaja katika akili zake, akarudi na kusema jamani sijui mnanielewa.. na ni makanisa mazuri tu yako kwenye very strategic place na majengo kabisa, sasa kwahiyo kutokea sasa na kuendelea, ngoja tumemaliza maziko.
Naa nashukuru Mungu nimepata taarifa, kule kwenye msiba nimetuma mwakilishi, mimi nimbeaki hapa tu kwa sababu ya ugeni wa kitaifa ambao tumeupokea hapa jana, ya kamati kuu ya kanisa la Assmblies of God kutoka Rwanda, ambao waliomba tokea mwaka jana kuja Tanzania, kujifunza namna ya ueneshaji wa kanisa.
Na tumekuwa tunapata hizi timu kutoka dunia nzima, wanakuja hapa kujifunza kama darasa, kwahiyo askofu mkuu yupo hapa na kamati yake yote imeshindikana kuondoka kwenda kwenye msiba, lakini ningekuwa kule tangu jana.
Jana tumefanya mapokezi na leo tumekuwa nao hapa, na kesho tunaendelea nao, lakini nimetuma timu kule, nimetuma askofu aliyenitangulia Mwanisongole aende msibani aniwakilishe, atoe salamu za Assemblies of God na kutoa rambirambi, naa pia amefanya kazi nzuri. Na kabla ya kuja hapa, nimeongea ne anasema shughuli zote zimekwenda vizuri, na maazishi yote yamekwenda vizuri, kwahiyo tutaendelea na huu uvumilivu lakini pia tutakaa na kuona labda wenzetu watakuwa tayari kurudi tena kwenye mapatano nje ya mahakama, sisi we are open, hatupendi vurugu, hatupendi uadui au ugomvi wa aina yoyote ule, na hatutaki kurudi tena kule tulikotoka.
No comments
Post a Comment