Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 11, 2013

MAKUMI ELFU WAJITOKEZA KUIOMBEA SYRIA AMANI


Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye maombi ya kufunga ya masaa manne kwa ajili ya taifa la Syria. ©AP
Makumi elfu ya watu walijitokeza siku ya Jumamosi katika kuitikia wito wa Papa Francis, ili kuombea amani taifa la Syria, ambalo limekuwA katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, ambapo na kwa sasa Marekani wanataka kushambulia taifa hilo kutokana na kusadikika kutumia silaha za sumu huko Damascus mnamo Agosti 21.

Papa Francis alitumia wasaha huo kuomba kimya kimya, ambapo wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro walibeba bendera za Syria pamoja na vipeperushi vilivyosomeka, "Achaneni na Syria", mengine yakisomeka, "Msiishambulie Syria".

Maombi haya yaliyotangazwa na Papa tarehe mosi Septemba, yaliitikiwa na maaskofu maeneo mbalimbali kuanzia Italy, Cuba, na sehemu nyinginezo, ambapo pia huko Damascus, mufti mkuu alimshukuru Papa kwa jitihada zake na kuwaalika waislamu kufunga na kuomba kwa pamoja na wenzao walioko Roma.
Papa Francis akiendelea kusali kwenye mfungo huo wa wa kuiombea Syria. ©AP
"Wahindu, Wabuddha, na hata wasio na dini wote walijitokeza kufunga kwa ajili ya suala hilo. haya ni mafanikio makubwa sana". Anasema mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Anata.

Vatican imekadiria takriban ya watu laki moja wamehudhuria maombi hayo ya mfungo, katika kumlilia Mungu aingilie kati hali mbaya inayoendelea nchini Syria.

Rais Obama anasubiria ridhaa ya Congress ili kupeleka majeshi yake nchini Syria, huku Ufaransa akimuunga mkono na kuwa tayari kufanya hivyo, ilhali mkutano wa nchi tajiri uliokutana St. Petersburg nchini Urusi ulionyesha mgawanyiko wa dhahiri ambapo Rais Vladimir Putin ameitaka Marekani kutofanya shambulizi, na kwamba hawatoiacha Syria peke yake.
Habari kwa hisani ya Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment