Writen by
sadataley
11:20 AM
-
0
Comments
Aliyasema hayo jana wakati ufunguzi wa kongamano la kimataifa la Haki Ardhi kwa Amani Endelevu, lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili al Kilutheri Tanzania (KKKT) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu) na kufanyika ijini Dar es Salaam.
Alisema sheria ya mwaka 1999 inaeleza umikili wa ardhi na jinsi ambavyo mwekezaji anaweza kumiliki ardhi na hakuna mageni anayeruhisiwa kutwaa ardhi ya Tanzania bali kumilikia kwa kipindi cha miaka 33 au 99.
“Tuna sheria nzuri za usimamizi wa ardhi, tatizo lipo kwenye usimamizi wenye jukumu la kusimamia wameacha mianya ya kuruhusu migogoro ya ardhi baina ya mtu na mtu na kundi na kundi…serikali inajitahidikukabiliana nayo kwa kutoa elimu na kushirikisha wananchi,” alisema.
Alisema nchi za Afrika ndizo zenye ardhi kubwa ambayo haijaendelezwa na ndiyo maana nchi za Magharibi zinakimbilia kwa ajili ya uwekezaji baadhi wakitaka kupewa mapande makubwa ya ardhi kwa ajili ya kujipatia mikopo kwenye benki na kutoendeleza maeneo husika na wengine wanaendeleza.
Alisema wawekezaji wengi wanahitaji ardhi kwa ajili ya kilimo na kwamba serikali imepitisha maamuzi ya kutotoa zaidi ya hekta 20,000 kwa mwekezaji na kumtaka aliendeleza kwa mujibu wa mkataba.
“Ipo hofu kubwa ya ardhi ya Tanzania kuuzwa kwa wageni, napenda kuwaambia Watanzania kuwa serikali iko makini na hakuna ardhi itakayopewa mwekezaji pasipo ukomo wa umiliki, sheria, kanuni na taratibu zipo na anayeshindwa kuendeleza hatua zinachukuliwa kulinda ardhi ya Watanzania,” alisema na kulipongeza kanisa hilo kwa kuamua kujadili rasilimali ardhi na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwa kujikita kwenye kujadilia masuala mbalimbali yenye kuisaidia serikali na kupeleka mapendekezo ya jinsi ya kutatua tatizo la msingi.
Alisema Tanzania ina eneo lenye ukubwa kilomita za mraba 945,087, eneo linalofaa kwa kilimo na mifugo ni kilomita za mraba 620,227 huku kilomita za mraba 440,000 hazijaendelezwa na kilomita za mraba 100,000zimeendelezwa kwa kilimo cha mazao, eneo la kilimo cha umwagiliji ni kilomita za mraba 290,000.
“Migogoro baina ya wakulima na wafugaji imekuwepo kwa muda mrefu sababu kuu zikiwa ni ufugaji wa kuhamahama, idadi kubwa ya mifugo, ukosefu wa elimu, mabadiliko ya hali ya hewa, upanuzi wa maeneo ya kilimo na makazi, upanuzi wa maeneo ya hifadhi za Taifa na usimamizi hafifu wa sheria,” alibainisha.
Alisema katika kukabiliana na migogoro hiyo ambayo imekuwa viashiria vya uvunjifu wa amani, serikali inatoa elimu kwa wakulima na wafugaji, kuandaa mpango wa matumzi ya ardhi ngazi ya vijiji na wilaya na kitaifa.
Awali, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Askofu.Dk. Stephen Munga, alisema pamoja na kukaribisha wawekezaji kwa ajili ya kuendeleza ardhi, lakinini lazima kipaumbele kiwe kwa wenyeji na jinsia wanavyonufaika.
Alisema hali ilivyo kwa sasa nchini ni mwenye fedha kuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kubwa kwa kadri ya matakwa yake huku mtu wa chini akishindwa kumiliki ardhi na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya sheria ya kumiliki ardhi.
SOURCE: NIPASHE
No comments
Post a Comment