Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 11, 2013

KKKT yataka suluhu ya haraka migogoro ya ardhi nchini


Kanisa la Kiinjili na Kilutheri KKKT limeitaka serikali kutafuta suluhu ya kudumu ya migogoro ya ardhi inayolikabili taifa ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kutokana na migongano ya ardhi miongoni mwa wananchi.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa Afrika itagharimika kiasi cha dola bilioni 4.5 kipindi cha miaka kumi kurekebisha madhara yaliyotokana na vitendo vya ugawaji ardhi kiholela kwa wageni.

Benki ya Dunia inaitaja Tanzania katika ripoti zake za uchumi kuwa ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa kutoa kiholela ardhi kwa wageni tena katika mchakato usiokuwa na uwazi ambao unazidisha umasikini hasa kwenye maeneo ya vijijini.

Takwimu kama hizo zinawapa wasiwasi wananchi na wanajamii wengine juu ya nafasi ya wazawa katika kunufaika na rasilimali hiyo

Pamoja na hasara hiyo ya kiuchumi, amani ya nchini nayo inakuwa mashakani kutokana na mapambano ya kuwania ardhi ikiwa ni pamoja na mapigano ya wakulima na wafugaji.

Kamati hiyo kupitia Taasisi ya Haki na Amani ya Sebastian Kolowa imeandaa kongamano kubwa la kitaifa litakalofanyika wiki ijayo litakaloangazia migogoro ya ardhi na utatuzi wake.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment