Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 3, 2013

MAOMBI YA KUFUNGA KWA AJILI YA SYRIA KUONGOZWA NA PAPA

Papa Francis akizungumza na waumini kuhusu Syria, ambapo amewaasa kumuunga mkono kuhusu kufunga na kuomba kwa ajili ya taifa hilo ambalo liko kwenye machafuko kwa muda sasa. ©AP
"Moyo wangu umeumizwa sana na kile kinachoendelea Syria, na kusononeshwa na taarifa zinazoendela hivi sasa". 

Ni kauli ya Papa Francis wakati akizungumza kwenye kibaraza cha St Peters jijini Roma siku Jumapili.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki ameeleza kusikitishwa na mauaji yanayotajwa kuwa yametokana na matumizi ya silaha zenye sumu, na kutaka pande zote zinazopigana kuweka silaha chini na kupatana kwa njia ya mazungumzo.

Makumi elfu ya watu walikuwa wakimsikiliza na kumpigia makofi kama ishara ya kukubaliana naye, wakati ambapo Marekani ameonyesha nia ya kutumia nguvu za kijeshi, ilhali taifa la Ufaransa likiunga mkono moja kwa moja hoja ya kutumia jeshi.

"Ninalaani vikali matumizi ya silaha za sumu. Nawaambia picha mbaya zinauchoma moyo wangu na akili yangu" alisema Papa akizungumzia picha na video za waathirika wa silaha za sumu zilizotumika Stria.

Baadhi ya waumini wakaliki wakifuatilia kwa makini asemacho Papa Francis kupitia runinga kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro. ©AP

Papa alitumia fursa hiyo kukumbusha umati wa watu kuwa kuna hukumu ya Mungu na hakuna anayeweza kuikwepa.

Kufuatia hali ya hatari ya kuzuka kwa vita zaidi na zaidi, Papa ameitangaza Jumamosi ya Septemba 7 kuwa siku maalum ya kufunga na kuomba kwa ajili ya Syria, na kuwaasa wakatoliki na wakristo wengine kujumuika naye siku hiyo kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro (St. Peter's Square)

"Dunia inahitaji ishara ya amani na kusikia maneno ya matumaini na amani". Alisema Papa Francis na kuiambia halaiki kuwa watakutana pamoja kuanzia saa moja jioni hadi saa sita usiku kwenye viwanja hivyo ili kupaza sauti zao.

Syria iko kwenye hatihati ya kushambuliwa na Marekani ambapo Rais Obama anasubiri ridhaa ya Congress ili apeleke jeshi kutokana na serikali ya Bashar al-Assad kusadikika kutumia silaha zenye sumu, ambapo zaidi ya watu elfu moja wamefariki dunia. Machafuko ya Syria baina ya Serikali na wapinzani wa Rais al-Assad yameacha mamilioni ya watu bila makazi, huku ikiripotiwa kuwa zaidi ya watu laki moja wamefariki dunia.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment